Nia ya Gwajima ni kushawishi Vyombo vya ulinzi kuichukia Serikali japo ameshafeli

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Ukisikiliza maneno yake katikati ya mstari kama mwanasaikolojia utagundua mambo mawili au matatu
1-Kujinyenyekeza kwa vyombo vya ulinzi na usalama na kujionesha kuwa ni mtetezi.
2-Kuhadaa wanaohudumu kwenye vyombo hivyo kana kwamba ana ubunifu wa namna ya kuvifanya viwe na maisha bora zaidi.
3-Kujidai kuwa haogopi kuvisema vyombo vya dola

Hii ni hadaa yenye uhaini ndani yake.
 
Ukisikiliza maneno yake katikati ya mstari kama mwanasaikolojia utagundua mambo mawili au matatu
1-Kujinyenyekeza kwa vyombo vya ulinzi na usalama na kujionesha kuwa ni mtetezi.
2-Kuhadaa wanaohudumu kwenye vyombo hivyo kana kwamba ana ubunifu wa namna ya kuvifanya viwe na maisha bora zaidi.
3-Kujidai kuwa haogopi kuvisema vyombo vya dola

hii ni hadaa yente uhaini ndani yake.
Kuna watu wanajifanya wanapigania haki na demokrasia lakini hapohapo wanataka utawala wa kijeshi.

Hawa mimi siwaelewi kabisa wanavyo ji contradict.

Utawala wa kijeshi ni wa kijeshi, ni wa amri, hauchaguliwi kidemokrasia. Una suspend katiba.

Hutakiwi kuwa mwanademokrasia halafu hapo hapo unataka utawala wa kijeshi.

That is a contradiction.

Matatizo ya elimu finyu, uongouongo na uvivu wa kufikiri.
 
Neno “uhaini” mmeanza kulichukulia poa these last 5 years. Hivi mnaelewa maana ya uhaini nyie?

Acheni hii mizaha hatarishi na ushabiki maandazi
 
Ukisikiliza maneno yake katikati ya mstari kama mwanasaikolojia utagundua mambo mawili au matatu
1-Kujinyenyekeza kwa vyombo vya ulinzi na usalama na kujionesha kuwa ni mtetezi.
2-Kuhadaa wanaohudumu kwenye vyombo hivyo kana kwamba ana ubunifu wa namna ya kuvifanya viwe na maisha bora zaidi.
3-Kujidai kuwa haogopi kuvisema vyombo vya dola

hii ni hadaa yente uhaini ndani yake.
Wewe ndo mkalimani wa Gwajima??.
Au unawashwawashwa tu.???
 
Pamoja na kubadilisha jina la ID lakini bado fikra zako zinaishi kwenye ile ID ya mwanzo...

Hayo aliyoyaongea, ingekuwa hoja hizo kazitoa ndani ya bunge ungeliita ni uhaini?

Ukisikiliza maneno yake katikati ya mstari kama mwanasaikolojia utagundua mambo mawili au matatu
1-Kujinyenyekeza kwa vyombo vya ulinzi na usalama na kujionesha kuwa ni mtetezi.
2-Kuhadaa wanaohudumu kwenye vyombo hivyo kana kwamba ana ubunifu wa namna ya kuvifanya viwe na maisha bora zaidi.
3-Kujidai kuwa haogopi kuvisema vyombo vya dola

hii ni hadaa yente uhaini ndani yake.
 
Wewe unajuaje kama yeye siyo "member' wa hivyo vyombo? Badala ya kuchukulia kama hadaa linaweza kuwa onyo, au tahadhali kabla ya hatari.

Power aliyonayo rais hazaliwi nayo, anayo mamlaka as long as watu wameamua kumpa hayo mamlaka na kumtii. Wanao uwezo wa kumkwida na kumweka mtu kati. Kisha ikatoka barua kuwa ameng'atuka na hakuna anachoweza kufanya.
 
Duuuh
 
Ukisikiliza maneno yake katikati ya mstari kama mwanasaikolojia utagundua mambo mawili au matatu
1-Kujinyenyekeza kwa vyombo vya ulinzi na usalama na kujionesha kuwa ni mtetezi.
2-Kuhadaa wanaohudumu kwenye vyombo hivyo kana kwamba ana ubunifu wa namna ya kuvifanya viwe na maisha bora zaidi.
3-Kujidai kuwa haogopi kuvisema vyombo vya dola

hii ni hadaa yente uhaini ndani yake.
Una akili ndogo sana sana wewe na ni kiazi haswaa! Taifa lina watu wenye ujinga sana sana na wengi ni wafuasi wa CCM sijui kuna shida gani huko CCM
 
Sasa unatuuliza sisi funaku ili iweje.. Jibuni hoja zake kwanza
 
Una akili ndogo sana sana wewe na ni kiazi haswaa! Taifa lina watu wenye ujinga sana sana na wengi ni wafuasi wa CCM sijui kuna shida gani huko CCM
Hiyo ndio think tank ya chama chawala
 
Nilichoelewa kwa Askofu Gwajima.

Ni nchi iwe na taasisi imara. Mfano nchi kama Marekani, kwa akili za Trump bila kuwa na taasisi imara angeleta madhara makubwa sana.

Hivi vinchi vyetu bahati mbaya tatizo lipo kwenye taasisi dhaifu.

Imewahi kutokea Igp anapangiwa kazi nyingine kama ubalozi,na ukichunguza ni kitofautiana kwenye utendaji.
Eneo kingine uteuzi wa majaji, mfano Kuna majaji waliteuliwa kutoka ngazi ya uhakimu kisa wamewafunga wapinzani haswa kipindi cha awamu ya tano. Kama nakumbuka vizuri kuna hakimu alimfunga Sugu,hatua iliyomfurahisha Jiwe na baadaye alipandishwa cheo na kuwa Jaji,sasa unategemea ataegemea wapi ikitokea shauri lenye maslahi ya watawala!

Uwe kama aliyepita watu wanapigwa eneo la mahakama yeye yuko kimya. Lakini ukiangalia alivyopatikana ni kama Cj wa kwanza kukaimu nafasi ya uCj kwa muda mrefu Sasa huwa Kwa njia aliyoipitia ni lazima aegemee kwa watawala zaidi.
 
Ukisikiliza maneno yake katikati ya mstari kama mwanasaikolojia utagundua mambo mawili au matatu
1-Kujinyenyekeza kwa vyombo vya ulinzi na usalama na kujionesha kuwa ni mtetezi.
2-Kuhadaa wanaohudumu kwenye vyombo hivyo kana kwamba ana ubunifu wa namna ya kuvifanya viwe na maisha bora zaidi.
3-Kujidai kuwa haogopi kuvisema vyombo vya dola

hii ni hadaa yente uhaini ndani yake.
Umejaza matope kichwan?
 
Kwa msimamo wangu, napinga tafsiri yako kwa sababu siyo tafsiri ya haki, haijazingatia muktadha wa mazungumzo, na kwa kweli haijajengwa juu ya hoja bali juu ya hisia na mashaka ya mtu binafsi.

Kama mtu ninayefikiri kwa uhuru, siwezi kuona kosa la mtu kuzungumza kwa heshima mbele ya vyombo vya dola. Kuonyesha heshima si kujipendekeza. Tunapaswa kutofautisha kati ya unafiki na ustaarabu. Si kila anayeheshimu taasisi ni mnafiki. Si kila anayesema jambo zuri kwa polisi, jeshi, au taasisi nyingine ni mtu wa hila. Huo ni mtazamo wa mashaka usio na msingi wa haki.

Vilevile, si sahihi kusema kuwa mtu anapotoa wazo la namna ya kuboresha maisha ya askari basi anawahadaa. Kutoa wazo ni sehemu ya haki ya kikatiba. Mtu anaweza kuwa na ndoto au mtazamo kuhusu mabadiliko hata kama hayapo mikononi mwake kuyatekeleza. Tunapochukulia kila wazo kama mtego wa kisiasa, basi tunazima uwezo wetu wa kukua kama jamii inayopokea fikra tofauti.

Halafu, kuhusu kusema kuwa gwajima hajaficha woga wake dhidi ya taasisi za dola, hiyo siyo dhambi. Huo ni mtazamo. Siyo kila anayesema bila hofu ni mchochezi. Taifa lisilo na nafasi ya kusema ukweli bila woga ni taifa linalozalisha wanafiki. Sitarajii jamii iwe na watu waoga ili tu waonekane watiifu.

Kwa hiyo, tafsiri inayoonesha kuwa hayo maneno ni ya hadaa yenye uhaini ndani yake, mimi naiita tafsiri yenye makosa ya kiakili na kiuono wa kihoja. Inajengwa juu ya tafsiri ya mtu na si kweli ya kauli yenyewe. Tafsiri ya namna hii ni hatari kwa sababu haijengi hoja, inazaa chuki, hofu, na hisia zisizo na msingi.

Sitetei mtu, ninatetea haki ya tafsiri ya haki. Sitetei kauli yoyote kwa upofu, lakini sitakubali pia ielezwe kwa upotoshaji wa makusudi. Tafsiri isiyo na mizizi ya hoja ni sawa na hukumu isiyo na ushahidi.

=> Kukubaliana na mtu si lazima, lakini kumtendea haki ni wajibu wa maadili. Msiompendea Gwajima ni haki yenu, lakini tafsirini alichosema kwa hoja, si kwa hofu wala chuki
 
Kuna watu wanajifanya wanapigania haki na demokrasia lakini hapohapo wanataka utawala wa kijeshi.

Hawa mimi siwaelewi kabisa wanavyo ji contradict.

Utawala wa kijeshi ni wa kijeshi, ni wa amri, hauchaguliwi kidemokrasia. Una suspend katiba.

Hutakiwi kuwa mwanademokrasia halafu hapo hapo unataka utawala wa kijeshi.

That is a contradiction.

Matatizo ya elimu finyu, uongouongo na uvivu wa kufikiri.
Sasa haya yanayotokea,

Mtu achukuliwe peupe na watu waliojitambulisha kuwa ni askari, wamkamate mtu, wamtie pingu Kisha kesho yake akutwe ameuwawa,

Huo ni utawala wa kikatiba au utawala wa kijeshi?

Nasubiri JIBU!
 
Ukisikiliza maneno yake katikati ya mstari kama mwanasaikolojia utagundua mambo mawili au matatu
1-Kujinyenyekeza kwa vyombo vya ulinzi na usalama na kujionesha kuwa ni mtetezi.
2-Kuhadaa wanaohudumu kwenye vyombo hivyo kana kwamba ana ubunifu wa namna ya kuvifanya viwe na maisha bora zaidi.
3-Kujidai kuwa haogopi kuvisema vyombo vya dola

hii ni hadaa yente uhaini ndani yake.
AWE MSTAARABU GWAJIMAAA,AWE MSTAARABU BIASHARA YAKE YA UTAPELI IMESHAISHA PALEE
 
Nilichoelewa kwa Askofu Gwajima.
Ni nchi iwe na taasisi imara. Mfano nchi kama Marekani, kwa akili za Trump bila kuwa na taasisi imara angeleta madhara makubwa sana.
Hivi vinchi vyetu bahati mbaya tatizo lipo kwenye taasisi dhaifu.
Imewahi kutokea Igp anapangiwa kazi nyingine kama ubalozi,na ukichunguza ni kitofautiana kwenye utendaji.
Eneo kingine uteuzi wa majaji, mfano Kuna majaji waliteuliwa kutoka ngazi ya uhakimu kisa wamewafunga wapinzani haswa kipindi cha awamu ya tano. Kama nakumbuka vizuri kuna hakimu alimfunga Sugu,hatua iliyomfurahisha Jiwe na baadaye alipandishwa cheo na kuwa Jaji,sasa unategemea ataegemea wapi ikitokea shauri lenye maslahi ya watawala!!
Uwe kama aliyepita watu wanapigwa eneo la mahakama yeye yuko kimya. Lakini ukiangalia alivyopatikana ni kama Cj wa kwanza kukaimu nafasi ya uCj kwa muda mrefu Sasa huwa Kwa njia aliyoipitia ni lazima aegemee kwa watawala zaidi.
Uteuzi wowote ule lqzima mtu atahusika kuteua na huyo mtu/ watu lazima ana mapenzi yake ambayo kwa namna moja au nyingine yanaathiri integrity, hakuna mfumo katika nchi yeyote duniani unaoweza kuwa ni imara kiasi cha kutopenyeka na ushabiki. Hata Marekani unayoisifia majaji wanateuliwa kwq mlengo wao kutegemeana chama kipi kina ⁹majority katika senate na hata nafasi zingine inategemea na chama kipi kina majority katika Congress.

Ungekuwa sio mtu wa kudandia mambo ungekuwa unaelewa huko duniani kukoje. Israel waziri mkuu Netanyahu anashtakiwq kwa makosa matatu ya rushwa lakini ni scheme iliyotengenezwa na mahasimu wake kisiasa muda mrefu ili kumng'oa madarakani.

Ni kama hapa kwetu utegemee kiongozi wa Chama cha mpira FAT asiwe mshabiki wa ama Yanga au Simba.

Watu wa aina moja huwa wana tabia ya kulinda maslahi yao, kuna wakati hapa tulikuwa na bunge la vyama vingi lakini lilipokuja suala la kuongeza maslahi yao wote kwa pamoja walipitisha kwa kukubaliana bila hata mmoja kupinga.

Eti unazungumzia hakimu kuteuliwa jaji kwa akili yako unafikiri majaji wanateuliwa kutoka wapi? Majaji wanateuliwa kutoka tasnia zote za sheria lakini majority wanatoka kwenye uhakimu na wachache wanatoka kama uendesha mashtaka, uwakili. Uchunguzi wa mashtaka nk.
 
Back
Top Bottom