Nia ya kuua/ Malice aforethought

Nia ya kuua/ Malice aforethought

Decree Holder

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
2,559
Reaction score
3,745
NIA YA KUUA/ MALICE AFORETHOUGHT

Kuua kwa kukusudia (murder) adhabu yake ni moja tu kunyongwa mpaka kufa. Kuua bila kukusudia (manslaughter) adhabu yake ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, na adhabu ya chini inaweza kuwa kuachiwa huru. Hii inamaana kwamba unaweza kuua bila kukusudia na ukafungwa masaa matatu au ukaachiwa huru ni uamuzi wa Jaji kulingana na mazingira ya kesi.

Kuua kwa kukusudia (murder) kunahitaji mambo mawili tu muhimu:
1. Kitendo chenyewe cha kuua au kusababisha majeraha yatakayopelekea kifo.( actus reus)
2. Nia ovu ya kuua (Malice aforethought)

Kuua bila kukusudia kunahitaji element moja tu
1. Kitendo chenyewe cha kuua au kusababisha majeraha yatakayopelekea kifo. Kwenye kuua bila kukusudia hakuna haja ya nia ovu. Kukishakuwa na nia ovu inamaana ulikusudia Kuua.

JE UTAITAMBUAJE NIA YA KUUA

Jaji Mlacha katika Republic Vs Respicius Patrick @ Mtazangira & another case No 56 of 2018 ya mauaji ya mwanafunzi ya mwalimu Respicius, mahakama kuu ya Bukoba anasema muuaji hawezi kutangaza nia yake ya kuua, hawezi kusema ana nia ya kuua. Kujua kuwa mtu alikuwa na nia ya kuua mahakama inaangalia vitu vifuatavyo.
1. Aina ya silaha iliyotumika kuua
2. Namna muuaji alivyokuwa anasababisha majeraha.
3.Maneno aliyoyatamka muuaji wakati anaua
4. Mambo aliyoyafanya muuaji kabla au baada ya kuua.
5. Nk

Katika kesi ya hivi karibuni ya mauaji ya mwanafunzi wa shule ya Scholastica, Mahakama kuu ya Moshi. Mahakama inasema tunaangalia
1. Silaha iliyotumika kuua
2. Mambo aliyoyafanya muuaji baada ya kuua.

AINA YA SILAHA
Mwalimu wa Bukoba alitumia ukuni kumuadhibu mwanafunzi, mahakama ikasema alikuwa na nia ya kuua.
Mlinzi wa shule ya Scholastica alitumia panga kumpiga mwanafunzi mahakama ikasema alidhamiria kuua.

MAMBO ALIYOYAFANYA MUUAJI BAADA YA KUUA

Mlinzi wa shule ya Scholastica baada ya kuua alienda kutupa maiti mtoni.
Mwalimu Respicius alidanganya uongozi wa shule kuwa amemkabidhi Sperius kwa wazazi wake salama. Pia alikimbia kwenda kujificha polisi walipofika kumkamata

NAMNA MUUAJI ALIVYOKUWA ANASABABISHA MAJERAHA

Mwalimu Respicius wa Bukoba alikuwa anampiga mwanafunzi sehemu yoyote ile ya mawili.

Mlinzi wa Shule ya Scholastica alimpiga mwanafunzi na panga kichwani.

Soma Mlinzi asimulia alivyomuua mwanafunzi
 
Back
Top Bottom