Niache nitulie, usinitoe roho bure.

Niache nitulie, usinitoe roho bure.

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
Katu hapandi Farasi, yule mzoea Punda,
Mpenda kwenda kasi, mwendo pole humshinda,
Amezoweshwa fenesi, doriani lamshinda,
Sitokalifisha nafsi, nafanya ninayopenda,
Loo! Nina wasiwasi, kwa mambo yanavyo kwenda.


Nipe gongo ya kiasi, nipate ipiga funda,
Na miraa ya Ramisi, kwa ubani naifunda,
Initoe kusikusi, hata kipoe kidonda,
Niupate na wepesi, wa kumkabili nyonda,
Hivi ni kitu rahisi, kutamka "nakupenda"?


Niko na pepo za kusi, ni mbali ninapo kwenda,
Sitaki hino mikasi, ya hawa wacheza chunda,
Wenye kupendwa wakwasi, shida nzito huzishinda,
Akina kikaragosi, yetu tu yanatushinda,
Kuliani sina tasi, yu wapi wa kunipenda?


Waja wapo kifurusi, hawana kitu kupenda,
Ubishi kama tunusi, natafuta pa kupanda,
Asojali mafurusi, ndiye nitakaye mpenda,
Mwenye kujali nafsi, na mafurusi kuyaponda,
Mapenzi ya wasiwasi, wallahi ni kama donda.



Moyo una wasiwasi, akili i'njia panda,
Huyu mja Ibilisi, ni jini msaka tenda,
Kila siku alhamisi, kwake siku huganda,
Si kuna siku nyepesi, na za kukaza mkanda?
kuna siku za mafurusi, na za mifuko kukonda.


Hili jua la utosi, halichagui la kumtenda,
Hata mwenye ukwasi, pia laweza mponda,
Ya jini kuhama rasi, pale kiti anapo konda,
Mwayaiga pasi wasi, ya majini mwayatenda,
Kwa tindo na bisibisi, mioyo mnaitinda.


Sina hofu sina wasi, tena nenda mwana kwenda,

Kitu changu kimepasi, hakiyumbi kimedinda,
Hupati tena nafasi, dagaa zangu kutanda,
Umeshakuwa unyasi, nyoka alo nipa donda,
Nimestuka kirahisi, we endelea kutanda.


Njano5.

0784845394.
 
Back
Top Bottom