Jabbzbbajja
Kaka mimi niko na swali nahitaji unisaidie majibu yake kama itawezekana,niko nampangi wakuja dubai soon kutafuta maisha,sasa kuna mtu aliniambia kua huko dubai kuna sehemu ambayo unaweza kupata nyumba za bei rahisi ambazo unaweza ukapanga yani ziko kama hostel unakuta kuna kitanda na godoro wewe unaenda na begi lako tu then kwenye chumba kimoja mnaweza mkawa mnashea watu watatu au wanne inategemea na hio hotel jinsi ilivyo then unalipia kama ni mwezi mmoja au miwili alafu unaishi hapo,sasa nilikua nahitaji kujua kuhusu hizo nyumba zinapopatikana maeneo gani au katika mji gani pia na usalama wake kiujumla maana kwenda kukaa room moja na watu ambao hamjuani mmekutana tu kwa mara ya kwanza nayo ni tatizo .