Niambie by Harmonize...

Niambie by Harmonize...

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
55,727
Reaction score
123,094
Leo nimebahatika kuangalia video ya huu wimbo, niambie. Nikisikiliza maneno nasikia umenipendea nini ingali sina dough(pesa). Mara mangi asije kukudanganya na kilo ya unga. Sina kazi hata senti tano kipande.

Sasa najiuliza mtu gani ana shida anaishi maisha ya kwenye hio video? Hayo magari,majumba kweli ni maisha ya mtu asie na hela? Anapoteza muda kwa kucheza tennis, hio racket ya tennis masikini hawezi kununua achilia mbali membership ya tennis club! Mwanamke unaeishi nae humo akiliwa na muuza genge sio kwasababu ya pesa.

Haya ndio mambo ya bongo movie jambazi anavua viatu mlangoni. Hamna washauri au ndio wamekariri video lazima iwe na nyumba na magari mazuri?

Ivyo vitu n mali ya demu sio harmonizer so demu alikuwa ni wakishua ila Harmo ni choka mbaya anaishi kwa demu
 
Angeonesha uhalisia wa maisha yake angeeleweka zaidi....
 
Video za wasanii wetu lazima ziwe na magari na majumba ya kifahari,manguo ya rangi rangi bila kusahau mabinti na vichupi ukitoa video bila ivyo vitu ukafuata uhalisia wa ulichoimba wenye timu zao lazima wakushambulie.
NIAMBIE audio ni tofauti na video watapambana hapa ku-justify eti alikua mariooo ila hakuna sehemu kasema vile vitu ni vya binti [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii ngoma pamoja na video yake vina maana kubwa sana kwa maisha ya wote wawili...

Mosi, ni kweli Wolper alienda kwa Harmonize wakati Harmonize akiwa hana kitu ingawaje kwa mbali alishaanza kunukia mavumba

Pili, wakati Harmonize anajiandaa kuachia hiyo ngoma waka-fake kuachana...

Tatu, baada ya muda mfupi wa tangu kuachiwa hiyo ngoma, drama za kuachana zikageuka kuwa sio drama tena bali reality!

Nne, inasemekana hivi sasa Harmonize yupo na demu mwenye mawe ya kutosha kama aliyojisingizia Wolper kwenye hiyo video!!!!
 
Leo nimebahatika kuangalia video ya huu wimbo, niambie. Nikisikiliza maneno nasikia umenipendea nini ingali sina dough(pesa). Mara mangi asije kukudanganya na kilo ya unga. Sina kazi hata senti tano kipande.

Sasa najiuliza mtu gani ana shida anaishi maisha ya kwenye hio video? Hayo magari,majumba kweli ni maisha ya mtu asie na hela? Anapoteza muda kwa kucheza tennis, hio racket ya tennis masikini hawezi kununua achilia mbali membership ya tennis club! Mwanamke unaeishi nae humo akiliwa na muuza genge sio kwasababu ya pesa.

Haya ndio mambo ya bongo movie jambazi anavua viatu mlangoni. Hamna washauri au ndio wamekariri video lazima iwe na nyumba na magari mazuri?

You nailed it.....ni upuuzi wa hali ya juu...maudhui ya wimbo hayaendani...na video....nawashauri...wawe wanafanya consultation kabla ya kutoa video...
 
Hii ngoma pamoja na video yake vina maana kubwa sana kwa maisha ya wote wawili...

Mosi, ni kweli Wolper alienda kwa Harmonize wakati Harmonize akiwa hana kitu ingawaje kwa mbali alishaanza kunukia mavumba

Pili, wakati Harmonize anajiandaa kuachia hiyo ngoma waka-fake kuachana...

Tatu, baada ya muda mfupi wa tangu kuachiwa hiyo ngoma, drama za kuachana zikageuka kuwa sio drama tena bali reality!

Nne, inasemekana hivi sasa Harmonize yupo na demu mwenye mawe ya kutosha kama aliyojisingizia Wolper kwenye hiyo video!!!!
Ila mimi naona video ingekuwa nzuri iwapo tungeona maisha ya Harmonize akiwa hana kitu, na upande wa pili akienda kwa huyo demu tuone anazo. Sasa video imeonesha maisha mazuri tu hamna hilo rhumba analoliimba. Inakuwaje awe na wasiwasi muuza duka atamuhonga kilo ya unga mwanamke tajiri hivyo?
 
Video za wasanii wetu lazima ziwe na magari na majumba ya kifahari,manguo ya rangi rangi bila kusahau mabinti na vichupi ukitoa video bila ivyo vitu ukafuata uhalisia wa ulichoimba wenye timu zao lazima wakushambulie.
NIAMBIE audio ni tofauti na video watapambana hapa ku-justify eti alikua mariooo ila hakuna sehemu kasema vile vitu ni vya binti [emoji23][emoji23][emoji23]
Hii video haiendani na anachoimba.
 
Ila mimi naona video ingekuwa nzuri iwapo tungeona maisha ya Harmonize akiwa hana kitu, na upande wa pili akienda kwa huyo demu tuone anazo. Sasa video imeonesha maisha mazuri tu hamna hilo rhumba analoliimba. Inakuwaje awe na wasiwasi muuza duka atamuhonga kilo ya unga mwanamke tajiri hivyo?
Hebu kwanza linganisha maudhui ya Niambie ya Harmonize na Zari la Mentali wa Profesa J!

Kwenye Zari la Mentali, Profesa J anaanza kwa kusimulia maisha yake akiwa ndani ya msoto hadi alipokutana na mtoto wa kishua!! Kutokana na hayo, video ina-flect maisha ya aina yote... wakati yupo ndani ya msoto na wakati alipokutana na mtoto wa kishua!!

Niambie haizungumzii maisha ya Harmo wakati akiwa ndani ya Msoto bali inazungumzia wakati tayari ameshakutana na mwanamke wa kishua na anaishi nae maisha ya kishua ambayo kimsingi ni ya huyo mwanamke!!!

Kwa maana nyingine, maisha anayoishi Harmo kwenye hiyo video ni yale yale ambayo aliyaishi Profesa J baada ya kuwa nae ameshakutana na mtoto wa kishua na kuishi nae pamoja. Mchakato sawa na ule wa Profesa J kukutana na mtoto wa kishua barabarani ulishapita kitambo na sio sehemu ya stori!!

Stori ni NIAMBIE, UMENIPENDEA NINI wakati hata kazi hana!!!

Video ingekuwa haina mantiki endapo tu wale wanawake wenye pesa wanapoamua kukaa na Mario basi ile hali aliyomkuta nayo mtaani, labda na kajinzi kake kamoja, huwa ataendelea kuwa nae akiwa hivyo hivyo hata kama alishamtoa kule vichochoroni na kuanza kuishi nae pamoja!!
 
Back
Top Bottom