Nianzie wapi kutafuta masoko ya nje?

GEOAFRICA

Member
Joined
Jan 30, 2019
Posts
14
Reaction score
11
Habari za humu jamani

Naombeni msaada wenu. Ninafanya biashara ya nguo za vitenge yaani nabuni nguo kisha nauza kwa watu kwa rejareja.

Ombi langu ni kwamba najaribu sana kupanua biashara yangu lakini sijui wapi nianzie. Natamani niwe na masoko sehemu mbalimbali kama vile Zanzibar, Uganda na kadhalika ila sijui nianzie wapi tafuta hayo masoko.
 
Ungeweka na sample zako humu huku wanaingia watu wa sehem mbali mbali ulozotaja😊 kila la heri
 
Nenda wizara ya biashara na uwekezaji utapata tips nyingi sana lakini pia ni vizuri kwenda field au eneo lenye soko lako lengwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chagua nguo ambazo unaziona ndo nzuri zaidi miongongoni mwa hizo unazozishona. Kwa ushauri target yako iwe wafanyabiashara wadogo au wa kati ndo hutapata usumbufu wa malipo. Unaweza kwenda Zambia ukaanzi tuseme Ndola, Kitwe na Lusaka na usisahau kufika Kamwala market kuna wabongo wengi wauza nguo watakushauri zaidi. Pia unaweza kwenda Kenya kwa kuanzia Mombasa na Malindi, kisha ukaenda Nairobi usisahau kufika sokoni Gikomba kuna wachaga wengi wauza ngu wanaweza kukupa mbinu za kupata wateja pale, kisha ukaenda Nakuru the Kisumu. Endelea na safari vuka mpaka nenda na uganda anzia Jinja kisha uende Kampala na Marara usikose kufika huko. Wakati wa kurudi pitia Masaka utapata wateja. N.B: Jifunze kua muongeaji mzuri.

Kila la kheri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anza kwa kujiunga na website za biashara za kimataifa kama vile tradekey. Com na alibaba. Com. Jiunge na taasisi kama Chambers of commerce huko huwa kuna fursa nyingi tu. Ila the best way ni kwenda kwenye maonesho ya biashara mwenyewe huko nchi za nje ili ujenge mahusiano ya uso kwa uso.
Natumia nimesaidia kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
asante sana ndugu yangu kwa masaada wako mzuri sana na nashukuru kwa kunionyesha njia na mwanga asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…