Nianzie wapi? nataka kuoa na kipato changu ni around 300k kwa mwezi

Hakuna kipato cha kutosha kwenye maisha. Hiyo 300k mkielewana na mkeo inatosha kusongesha maisha.
Zingatia neno mkielewana.
Hata mabilionea maisha ya kuwa na mke wengi wameshindwa.
Chukua jiko msaidiane kuongeza kipato.
 
Nao wanasema Olewa na mwanaume anakupendaπŸ˜†πŸ˜†
NB;NDOA NI UTAPELI,,NDOA NI KIFO,NDOA NI MSONGO WA MAWAZOπŸ˜†NDOA NI KULALA NA ADUI YAKO KITANDA KIMOJA HIVI HAMCHOKI KULALA NA MWANAMKE HUYO HUYO KILA SIKUπŸ˜†
Wapige za kichwa mkuu
BADO ANAPUMUA
NDOA NI KIFO
 
Gharama za maisha zinatofautiana na mahali ulipo,wale wahadzabe wa kule Manyara waliogeuka kuwa wa maonesho hata 100,000/mwezi hawana na wana familia.

Wewe oa tu,majibu ya maswali yako utayapata huko.

Huku kumejaa "Kataa ndoa" utajikuta huoi.
 
Zingatia ushauri wangu. Oa mkuu, Ila binti na awe ni bikra awe ametoka mikononi mwa wazazi na amelelewa vizuri kwa maadili. Hautojutia.

Nakusisitiza. Awe bikra.
 

Attachments

  • images (47).png
    12.4 KB · Views: 13
  • images - 2026-08-10T194656.412.jpeg
    28.3 KB · Views: 10
  • images - 2026-08-10T194352.388.jpeg
    21.7 KB · Views: 16
UKIWA BROKE NDIO KIPINDI KIZURI CHA KUPATA MKE MWEMA

nilimpata my wife nikiwa broke infact yeye alikuwa na uchumi mkubwa kuliko mimi,TUKAANZA WOTE FROM THR SCRATCH kuna wakati tulishindia mkate na chai tu...tukatembea wote katika shida na raha ,tumetafuta WOTE juani mpaka leo tulipo ni tofauti na tulipotoka.

SO inawezekana kupata mke mwema inawezekana KUOA hata kama BADO UNAJIPANGA kiuchumi,sio usubiri Mpaka UFANIKIWE UTOBE KIMAISHA ndio UOE.

OA MWANAMKE ANAYEKUPENDA
 
Sijui unaishi mji gani lakini yote hayo itategemea na mke wako, kama ana mambo mengi basi itakula kwako...wasikutishe watu Kwa Kusema subiri baada ya miaka miwili kipato kiongezeke, maisha ya kuanza sifuri hayapo hivyo kabisa, maisha ya kuanza moja hatua zake ni ndogo ndogo Sana, yaani ww kuja kupata pesa unayotaka ni baadae Sana, jiangalie je mm naweza kutunza mtoto wa mtu Kwa maana ya Chakula, malazi, mavazi, afya na vitu vidogo vidogo vya kifamilia, ukisema ndiyo Kwa dhati kabisa basi nenda kaoe kama unavyotaka tena kimbia haraka, hiyo 300K inatosha Sana Tu kwaajili ya familia na chenchi kidogo inabaki. Tena ww Kwa Hali yako Una nafasi nzuri ya kupata mke mwema.
 
1. Usioe kwa kufunga ndoa.
2. Tafuta binti asiye na njaa (ambaye hajatoka familia fukara) yaani wazazi watumishi wa umma).
Hii itakufanya uishi naye comfortable Bila usumbufu wa kupigiwa kuhusu matumizi na matatizo ya nyumbani kwao.

3. Ukishaishi naye, muanzishie biashara lakini ni baada ya kumjaza mimba ya kwanza.

4. Endelea kutafuta namna ya kuongeza channels ya kipato chako.

Miaka 28 ni michache lakini pia ni Mingi kwa kama hutokuwa makini kupanga safu ya mashambulizi yako kwani kutoka hapo mpaka miaka 40 sio mbali sana.
 
Usioe unless huyo mwanamke awe na ajira au kipato cha kudumu.
 
Mbona una ata tu JIKO lako freshy, kama tayari una geto lako una jitegemea hao umemaliza hatua ya kwanza, Mahari huwa sio kosa kudaiwa So wewe wapelekee wakwe zako ata mbuzi 2 tu kwanza, usiwe na sherehe we funga ndoa ata ya BOMANI kwanza then mengine mtayafanya mbele kwa mbele huko
 
Umri huo unaoa et cocomelon wa 98 hebu kula maisha tafuta hela kwani huwezi kuwa na mahusiano tu bila ndoa πŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›

For sure ni ngumu sana kuishi kwa kipato hiko halafu uwe na majukumu ya kulea usije ita watu wachawi wewe jipe tena miaka 5 mbele kama CR7 kaoa na 41
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…