Nianzishe biashara gani ili niweze kujikimu?

Don R

Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
17
Reaction score
4
Habarini wana JF

Mimi ni kijana wa miaka 20. Nilimaliza form 6 mwaka huu combination ya PCB nikapata div II. Ni kwamba hali yangu imekuwa ngumu mno hasa ktk kipindi hiki cha chuo kwa sababu mzee wangu binafsi ana uwezo wake mzuri tu wa kunisomesha hata miaka kumi sema alikataa kunisomesha na kuona kama ni mzigo kwake na kuamua kufanya biashara zake.

Sio hilo tu, hata matumizi yenyewe shule illikuwa mbinde na hela zipo. Sasa kiukweli binafsi inauma mno nikiona tu anatoa kwa watu wengine ambao sio wa kifamilia; sijui ni limbwata hata sielewi!

So nikapata bahati tu ya kusomeshwa na msamaria mmoja tu ila tu ana condition kali kinoma. Yani ni kwamba anakusomesha kwa mkopo ili baadae nije kumlipa nikiajiriwa na hapo hela inayotolewa ni ada tu maswala ya hostel na matumizi juu yako mwenyewe na kama ilivyo mzee hataki kunisaidia hata na mia yake.

Kwahiyo nilikuwa naomba ushauri wanaJF kwamba hii hela ya ada ya huyu jamaa anaenlipia ada niikate kidogo kama robo niweke kwenye biashara ya kujiajiri mwenyewe ili nijipatie hapo visenti vya kuishi?

Maana hapa naogopa mno nikifikiria ni hela ya watu nkianzisha biashara ikifa inakuwa jau tena au labda nianze biashara kama ipi yenye uhakika hela yke itarudi na faida kubwa?



NISAIDIENI WADAU HAPA CHUO SIWEZI KWENDA KWANZA NATAFUTA HIYO HELA YA HOSTEL KWANZA NA YA MATUMIZI!
 
Anyways, tushajua hajui kuandika bt je mna ushauri gani kwa mdogo wenu? Mpatieni ushauri au hamjaona juu kapasua div 2 ????! Ebu tuwe waungwana tumpe ushauri wa kujenga sio kubomoa
Ushauri gani tena apewe....? Zaidi ya huo wa kuandika!!!?
Form 6 kweliiii[emoji15]
 
Huna adabu ndiyo sababu baba yako kakunyima ada, namshauri akunyime kabisa kabisa maana unaonekana tabia mbaya na hujitambui, yaani hizo cwezi zako inapnesha huna adabu
 
Umeniudhi sana, ulivyoandika, na kama ungekuwa umeweka jina hapa ofisi hata kama ushauri usingepata kazi kabisa!

Niliona mameno haya kwa wadada, sasa hata wa kiume mnaandika! Komeni kabisa! na wengine wote acheni tabia za ki darasa la kwanza.

KUHUSU MAMBO YAKO! PCB hakuna combination unaweza kujisomesha kwa masomo hayo.

1. hangaika kupeleka wazo lako kwa viongozi wahusika mahali ulipo, wizara, TCU n.k ili wakupe mkopo usome. Ukisomea mambo ya afya huwezi kukosa kazi utalipa mkopo bila tabu.

2. Kama hilo huwezi hilo, Tuliza akili yako tafuta chako, PATA KAZI (TEMPORAL JOB) kuanzia kufundisha vijana, viwandani, n.k ili ukusanye fedha uende kwenye vyuo vya kati baadaye utaendelea mwenyewe. Wapo waliofanya hayo leo wapo vizuri!

3. Tuliza kichwa tena(hili ni gumu sana) fanya biashara kuanzia na mtaji mdogo sana, utakua kidogo kidogo na baadaye uende kama namba 2 hapo juu.

KIUJUMLA: Form six huna haja ya kulia lia sana kama mzazi yupo hivyo tafuta mbinu zingine! kama ulifauru f4, na f6 tumia akili kutafuta vyako
 
Mzazi wako yuko sahihi kabisa kama wewe ndo umesoma hiyo PCB (daktari mtarajiwa) ukamailiza hiyo fomu siksi na ukafaulu vizuri (maana sisi tusiyoenda shule tunaambiwa hiyo divisheni tu kwa pisibi si mchezo) lakini unachokiandika ndio hicho mispellings kibao, kiswahili kibovu, kiujumla uwasilishaji mbovu kabisa, braza hiyo shule nahisi ulienda kuongeza ujinga tu na si kuundoa

Form six huyo je wa form four au two sijui ataandika nn. Elimu yetu inahitaji kufanyiwa evaluation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…