Nianzishe biashara gani ili niweze kujikimu?

Nianzishe biashara gani ili niweze kujikimu?

Aisee chief hata kuandika tu hujui?

Hiyo PCB ulifaulu kwa namna gani? Nina mashaka na uaminifu wa NECTA.
 
kwanza nilijua wewe sio mtoto wangu, pili nilikuona kilaza toka unaanza kutambaa, baada ya kuanza kutambalia mgongo. nipo humu kijana
 
Hata miye ningekuwa mzazi wako kisha unaandika upumbavu kama hivyo, bora nikanunulie malaya aisee. Ukinywa bia unaweza kuongeza siku za kuishi kuliko kulipia ada punda kama hii
 
Nimegundua ni kwanini Tanzania haiendelei vyema, unaweza kuwa umetoka kucheza chandimu(mpira wa makaratasi), ukacharazwa viboko na mzazi kwanini umejichafua.
 
Acha uongo dogo
PCB
Div two
Ungeaply Medicine ungepata tena vyuo vya serikali na 100% mkopo plus bonus ya special fucult
Hizo ngojera kawaeleze fb.
 
Habarini wana JF

Mimi ni kijana wa miaka 20. Nilimaliza form 6 mwaka huu combination ya PCB nikapata div II. Ni kwamba hali yangu imekuwa ngumu mno hasa ktk kipindi hiki cha chuo kwa sababu mzee wangu binafsi ana uwezo wake mzuri tu wa kunisomesha hata miaka kumi sema alikataa kunisomesha na kuona kama ni mzigo kwake na kuamua kufanya biashara zake.

Sio hilo tu, hata matumizi yenyewe shule illikuwa mbinde na hela zipo. Sasa kiukweli binafsi inauma mno nikiona tu anatoa kwa watu wengine ambao sio wa kifamilia; sijui ni limbwata hata sielewi!

So nikapata bahati tu ya kusomeshwa na msamaria mmoja tu ila tu ana condition kali kinoma. Yani ni kwamba anakusomesha kwa mkopo ili baadae nije kumlipa nikiajiriwa na hapo hela inayotolewa ni ada tu maswala ya hostel na matumizi juu yako mwenyewe na kama ilivyo mzee hataki kunisaidia hata na mia yake.

Kwahiyo nilikuwa naomba ushauri wanaJF kwamba hii hela ya ada ya huyu jamaa anaenlipia ada niikate kidogo kama robo niweke kwenye biashara ya kujiajiri mwenyewe ili nijipatie hapo visenti vya kuishi?

Maana hapa naogopa mno nikifikiria ni hela ya watu nkianzisha biashara ikifa inakuwa jau tena au labda nianze biashara kama ipi yenye uhakika hela yke itarudi na faida kubwa?



NISAIDIENI WADAU HAPA CHUO SIWEZI KWENDA KWANZA NATAFUTA HIYO HELA YA HOSTEL KWANZA NA YA MATUMIZI!
Hiyo hela anayokupa huyo mtu kuna uwezekano mkubwa ndio pesa hiyo hiyo ya baba yako ila hataki wewe ujue kwa sababu zake binafsi.


Au huyo jamaa hana nia ya kukudai, anakusomesha tu ili uone uchungu wa pesa hatimaye usomw vizuri .
 
Anyways, tushajua hajui kuandika bt je mna ushauri gani kwa mdogo wenu? Mpatieni ushauri au hamjaona juu kapasua div 2 ????! Ebu tuwe waungwana tumpe ushauri wa kujenga sio kubomoa
Mzee baba jiulize kwanini baba ake kamkacha + mwandiko utajua unapoteza mda wako bure kushauri
 
Mimi binafsi sijaona bwana mdogo alipokosea, ila humu jf kila mtu anajifanya mjuaji, mnamwandama kijana wa watu kisa mwandiko

Nasemaje, acheni upumbavu wenu tukiwa peni na karatasi muandike hapa essay tuone mwandiko wenu tutakimbiana
 
Back
Top Bottom