NIC ni nini? Inafanyaje kazi?

NIC ni nini? Inafanyaje kazi?

J33

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
1,552
Reaction score
1,513
Wakuu heshima kwenu,

Ninataka kujua hii taasisi ni ya nini na inahusu nini hasa, Jirani yangu alijiunga na mfuko huo bila kuelewa kwa miaka zaidi ya kumi sasa wakawa wanamkata 24000 kwa mwezi, mwaka juzi mwanzoni wakamuita kuwa bima yake imeiva na wakampa check ya million mbili. Baada ya hapo wakaanza kumkata 46000.

Sasa jirani yangu huyu anastaafu ndani ya mwaka huu na amewafata NIC na wakamwambia Bima yake itaiva mwaka 2021.

Hii maana yake ni nini na huyu mfanyakazi anaweza kupataje haki yake? Ikumbukwe kwamba hawa wafanyakazi ni watu wa vijijini ambao ki msingi waliingia kwenye izi taasisi bila kujiandaa vya kutosha.
 
shirika la bima la taifa ilo.bima zipo mbali mbali.hapo walikata bima ya maisha huenda.sasa terms na conditions huenda hawakusoma wakaelewa au hawakusoma kabisa .ilo tatizo kubwa.ufupi apo kama hataki akatwe aende ofisini kwao afute mkataba nao .kuna form za kujaza .ingekua amefail kulipa ingefanyika breach of a contract
 
Dah......Katika mashirika ya umma ya hovyo NIC ni namba moja.....linaendeshwa na wakurugenzi waliolala fofofo... wapigaji wenye njaa kali....na waliojaa utapeli....haiwezekani mtu miaka 2 inapita tokea bima iive,,,na mtu hajalipwa malipo yake ....na bado wakurugenzi wanajilipa mishahara minono huku wakiendelea kufanyia mikutano yao ya bajeti Zanzibar kwenye mahoteli ghali huku wateja wao wanyonge wakitaabika.....mbona mashirika mengine binafsi yako vizuri na yanakuwa siku hadi siku??... Ningekuwa JPM ningewatumbulia mbali na kuwafikisha mahakamani......
 
Hawana hela za Kulipa Claims. Pesa wanazokusanya kutoka kwa wanachama ndo wanazotumia Kulipa Mishahara ya wafanyakazi wao. Hawana investment yoyote tegemea kabisa kutolipwa Milele.
 
Back
Top Bottom