mwanasiasa huyu muitaliano aliandika kitabu hiki mwaka 1513. kwa tuliokisoma tujuzane kanuni za humo ndani. Cc MALCOM LUMUMBA, MSEZA MKULU, nyumba kubwa
anasema watu wanatakiwa kutendewa wema au ubaya. na si katikati. ukiwatendea ubaya kidogo huwa wanalipiza kisasi ila ubaya ukiwa mkubwa hawawezi lipiza. hivyo kama unatenda ubaya, tenda mkubwa.
anasema. kama umevamia nchi/mji na uliwakuta watu wana uhuru, mila na desturi zao. ili uweze kuwatawala inabidi uwaache na uhuru wao au uharibu uo mji. tofauti na hapo ni kutafuta matatizo.
Anasema mtu mwenye hekima huiga wale waliofanikiwa. hata kama hana uwezo kama wao atafaidika.
Anasema awe kama mpiga mshale ili kupiga mbali anapiga kuelekea juu.
hapa anamwambia Rais kwamba. kuanzisha mfumo mpya ni kazi ngumu. walionufaika na wazamani watakupinga sana na wengine watakutetea kishingo upande sababu hawana uhakika na uwapelekako.
anasema kiongozi akiwa mkatili na anaogopwa anapaswa kukaa mbali na mali za raia wake ili asichukiwe. Anadai ni rahisi mtu kusahau mauaji ya baba yake kuliko akiporwa mali aliyoachiwa na baba yake.