Nichagulieni gari kwa bajeti ya Milioni 10

Udochi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
787
Reaction score
1,056
Shikamoni waheshimiwa,
Mimi sijawahi kumiliki gari tangu nizaliwe.

Kazi yangu ni kuuza duka la Mangi. Kipato changu ni wastani wa Laki 5 kwa mwezi (hakiko imara kabisa; kinaweza kupungua au kuongezeka kidogo kutegemea na hali ya biashara).

Nimedunduliza hela kwa miaka miwili nimepata milioni kumi. Lengo langu nipate gari la kutembelea mjini na mimi.

Sasa ninachoomba waheshimiwa, Nichagulieni gari kwa kuzingatia kipato changu hapo juu.

Kuna watu wataniuliza maswali ya kitaalamu hapa, Mara Injini silinda sita, mara cc za mafuta, Mimi sina ujuzi huo.

Mimi ninachotaka mnichagulie gari dogo lolote, Mimi nitaendesha tu ili mradi litoke Japan na mpaka kulipia gharama zote na kuanza kuliendesha kwa uhuru isizidi kiasi tajwa hapo juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nikushauri
Gari halinunuliwi kwa bajeti uliyonayo bali gari linanunuliwa kwa matumizi
Kabla huja fikiria hiyo bajeti jiulize matumizi ya hiyo gari unayotaka ni yapi je ni movement za mjini tu au ndio trip za shambani na mkoani
Kwa bajeti hiyo fresh from Japan utapata
Ist nzuri sana nadhani itakufaa
 
Binadamu bhana yaan mtu kaomba ushauri jinsi ya kununua gari mtu anashauri ufungue bishara kwan yeye amewambia anataka kufungua biashara
Anyway me sinauelewa kuhusu magar ngoja wenye nia waje wakupe mwongozo
Lakini sio mbaya mkuu, kwani lengo lao ni kutoa ushauri wa kimaendeleo, na wanafanya hivyo kwa upendo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamata paso utang'oa watoto wote wakari wakari tena kama huyu Bushmamy unamla ata kwa mkopo
 
Shukrani sana mheshimiwa. Mimi kwa sasa mizunguko yangu ni ya mjini tu. Kwenda mkoani ni mara moja kwa mwaka, ambapo nikiona gharama ya kwenda mkoani kwa usafiri binafsi ni kubwa naweza kwenda kwa usafiri wa umma tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…