Shikamoni waheshimiwa,
Mimi sijawahi kumiliki gari tangu nizaliwe.
Kazi yangu ni kuuza duka la Mangi,
Kipato changu ni wastani wa Laki 5 kwa mwezi (hakiko imara kabisa; kinaweza kupungua au kuongezeka kidogo kutegemea na hali ya biashara).
Nimedunduliza hela kwa miaka miwili nimepata milioni kumi.
Lengo langu nipate gari la kutembelea mjini na mimi.
Sasa ninachoomba waheshimiwa,
Nichagulieni gari kwa kuzingatia kipato changu hapo juu.
Kuna watu wataniuliza maswali ya kitaalamu hapa,
Mara Injini silinda sita, mara cc za mafuta,
Mimi sina ujuzi huo.
Mimi ninachotaka mnichagulie gari dogo lolote,
Mimi nitaendesha tu ili mradi litoke Japan na mpaka kulipia gharama zote na kuanza kuliendesha kwa uhuru isizidi kiasi tajwa hapo juu.
Sent using
Jamii Forums mobile app