Nichagulieni gari kwa bajeti ya Milioni 10

Kajenge tu ndugu yangu!...... Hayo magari sio issue saaaana
Malengo ya kujenga ninayo kabisa mkuu, ingawa nimepanga kujenga kwa awamu.
Nitadunduliza nikipata Milioni 2 naanza hatua 1, nadunduliza tena ikifika Milioni 2 naingia hatua ingine, kwa kuwa uwezo wa kujenga nyumba ikaisha kwa mara moja sina kwa kipato changu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii biashara kubwa umefanya research itakuhitaji mtaji wa shilingi ngapi, matazamio ya mapato yako kwenye hiyo biashara kubwa ni kama kiasi gani kwa siku au mwezi? @udochi

Sent using Jamii Forums mobile app
Biashara kubwa ninayoifikiria kwa hali yangu ni ya duka kubwa la dawa za binadamu, na ikiwezekana niwe nayo hata mawili, mjini 1 na kijijini 1.

Mtaji ni kuanzia Milioni 15,
Changamoto kubwa kwangu ni elimu ya hiyo biashara, na nilijaribu kumuulizia mtu anayefanya hiyo biashara yeye ana maduka ya dawa manne na ni daktari,
Kwa kuwa sina mazoea naye akaniambia kwa kifupi tu kuwa kwa kuwa mimi sina elimu hasa ya masuala ya dawa, itanipa shida sana kwenye usimamizi, kwani nitategemea kuwaajiri watu wanaojua.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
We unawawajua wachaga
Atakwambia nafanya vibarua vibarua huko mjini kumbe lakini ukimchunguza hizo biashara zake sasa
Huyo jamaa mshaurini tu maswala la gari na sio kumtoa akili anajua anachokifanya


Sent using Jamii Forums mobile app
Mheshimiwa,
Ndugu zetu wala hawana lengo la kunitoa akili, ila wapo katika kutoa mawazo yenye lengo la kunishauri kimaendeleo, na mawazo yao ni mazuri.

Nakushukuru sana kwa kusisitiza kuwa wasiache kunishauri kwenye Kipengele cha kupata usafiri ambao utaendana na kipato changu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwongo huyo kwani ye anakaa dukani anauza muda wote? Binadamu wanakatisha tamaa sana. Nakushauri ongeza hiyo mil 5 uanze na hilo moja ndo udundulize toka mangi shop+dawa ndio ununue gari.

Kwasababu ukinunua gari Leo itakuchukua tena miaka miwili kudunduliza upate pesa ya duka la ndoto yako.
Duka la dawa ulitaka kufungua mjini sehemu gani?
Kariakoo, au nje ya Kariakoo?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gari zote huwa zinakaguliwa kabla hazijaja na hiyo ni must

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi kwa ushauri kumbe hawa wabongo ni matapeli

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio matapeli ni wezi.
Utasikia ukiagiza kwetu gari utalochagua ndio litakuja huko kwingine waweza letewa gari bovu......

Magari yote lazima yakaguliwe ndio yanakuja tz.

Pia watakwambia kuwa gari imelipiwa kila kitu hadi registration wakati registration ni sehemu ya kodi unayolipa tra

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitalifikiria kwa kina hili wazo mkuu.

Lengo nifungue nje ya mji,
Maanake kwa mtaji huo sidhani kama naweza kufungua Kariakoo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio Kariakoo huwezi. Fanya hivyo tafuta location unayoiona itakulipa then njo nikupe kijana wangu akusaidie mawazo, mwaka ujao December uwaletee watu mrejesho. Kwani dawa zina faida sana sio tofauti na mangi shop au ni hobby?
Nitalifikiria kwa kina hili wazo mkuu.

Lengo nifungue nje ya mji,
Maanake kwa mtaji huo sidhani kama naweza kufungua Kariakoo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, huyo kijana ni mtu mwenye taalima ya uuzaji dawa?

Kuhusu suala la kuwa inalipa sina uhakika, ila nimeona kuwa kwenye upande wa afya kuna uhitaji mkubwa sana kwenye jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli unaweza kununua gari kwa mtu lenye gundu...unakuta gari lilikuwa linatumiwa na wahuni kama danguro la kugegeda wake za watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani mkuu hukumsikia Mh.Makonda kuhusu IST?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…