Nicheke au nilie?

Nicheke au nilie?

ila mkae mkujua kwa mila nyingine mke wa mtoto wa kiume kumwona baba wa mumewe akiwa uchi ni laana na akijua mumewe kuwa mkewe alimwona babake uchi italeta matatizo, kwa mtazamo wangu amwoondowe yule binti na asimeleze mumewe kabisa hicho kisa
 
ila mkae mkujua kwa mila nyingine mke wa mtoto wa kiume kumwona baba wa mumewe akiwa uchi ni laana na akijua mumewe kuwa mkewe alimwona babake uchi italeta matatizo, kwa mtazamo wangu amwoondowe yule binti na asimeleze mumewe kabisa hicho kisa

Naunga mkono hoja, sio heshima kumwambia mumewe kuwa kamuona b'mkwe akiwa mtupu, amtoe huyo house maid kimya kimya...
 
Ooh my God! Sijui ni laana au ndio urijali? Anyway huyo mzee ameshadhihirisha kapona kabisa. Hata mimi naunga hoja wazo la kumshirikisha Mwenzi wako. Lakin hebu tujiulize, asipokuamin na kusema hiyo ni njia yako ya kumfanya babake aondoke kwa kuwa umeumchoka utafanyaje?

Kwa kuwa ulishindwa kumwambia mumeo asubuhi ilele ili akajionee na macho yake, basi Plan B ni muhim. Rudisha binti kwao, halafu mpange safari ya kijijini (mwambie mumeo mkamtembelee mamamkwe) hapo kutakuwa hakuna jinsi Babamkwe hataweza kubaki peke yake.

Mkifika huko mnamuacha, halafu mkirudi ndio unamwambia mumeo kilichotokea

Hapo kwenye bold ndo issue, ila ni muelewa, ntajaribu. Asante kwa ushauri
 
ondoa huyo dada atatembea hata na mumeo huyo
kuhusu baba mkwe piga kimya maana akitolewa hapo ndo utaanza maneno na ndugu za mumeo oooh ulimfukuza baba yao mgonjwa .utayaweza
timua iyo changudoa
 
Sijiheshimu na sijatulia kivipi?Mbona mie hata hiyo avatar sijaiweka?Loh

Eti mwaya, mi mwenyewe nimerudi juu mara mbili mbili kuangalia hiyo avatar sijaona. Labda hajapenda jina la "Kipapatio" ndo anasema avatar.
 
dU!
Laana ya Dunia hii!
Mwambie Mumeo..huwezi kaa na jambo kama hilo peke yako...yeye ndo atajua jinsi ya kumwondoa baba yake...
Lakini hakikisha umebakiza ushahidi wa kutosha juu ya tuhuma hizo nzito, maana vinginevyo utaonekana umemchoka baba mkwe na unataka aondoke tu, na hii inaweza kuteteresha mahusiano ya nyumba yenu!
Sipati picha kitatokea nini kama mumewe pia alikuwa anajimegea huyo hausigelo....
 
ukimuondoa dada wa kazi, babu atakutaka wewe, la msingi mlete mamkwe after a week warudi bush.
 
ukimuondoa dada wa kazi, babu atakutaka wewe, la msingi mlete mamkwe after a week warudi bush.:shock:
  • A%20S%20embarassed.gif






 
HIYO NI LAANA MBAYA,
Mjulishe Mumeo Haraka, Lakini pia Huyo Binti kuwa mwangalifu sana nae, asije kuvunjia na nyumba yako

Hekima Itumike kumwondoa kwanza Baba ndipo uje ujue namna ya kumwondoa na Binti

Ikikosekana HEKIMA, Tatizo jingine linaweza zaliwa ktk Familia hiyo
 
duh... hii kweli bongo kupita unavyoijua... sasa kibabu cha miaka 70..!!! mimi na umri wangu umekwenda lakini huyo wa miaka 60 tu sitaki kumsikia.
Ningekua mimi ndio wewe, the same morning ningemuita mwanae aje ashukudie mwenyewe kwa macho yake. kumbuka yule ni baba yake mzazi, huwezi kujua ataichukulia vipi ukimwambia. anaweza asikuamini akichukulia baba ni mgonjwa na umri alionao. Sisi tulioolewa mara nyingi tunaonekana hatupendi upande wa waume zetu, hivyo unaweza kumwambia mumeo na asikuamini.
 
Naona nilijibu kwa kushangaa mpaka nikashindwa kukupa ushauri.
Kama walivyosema wengine naona, angalia jinsi ya kuongea na mumeo, binti wa miaka 16 ni mdogo sana, hilo libabu litakua limemdanganya tu. Babu arudi kwa mkewe aache kujifanya mgonjwa kisa ana baka vitoto vya watu.
 
The old man was ill. Now he is getting better. Let your house girl take care of him. After all that is why patients get well faster when looked after by pretty nurses.

Give him some room and he will leave in due time. Dont send him away. The least you can do is to call your mother in law to come and take care of hi.

dah madoctor wana ushauri mzuri kweli
 
mwache babu nae apate mashamushamu,duh ila dunia imeisha hicho kitoto cha miaka 16 kina tembea na mzee khaa,
 
Du! tumia akili kumuondoa huyo binti. Maana babamkwe anaweza kugeuka mwiba katika ndoa yako. Bila shaka unazijua tabia za mumeo na atakavyokuchukulia ukimweleza hili. Kama litavuruga mahusiano usimshirikishe, mtoe binti kwa sababu nyingine, hii ihifadhi moyoni.

namini nakubaliana na wewe,atunze rohoni alafu mpeleke kwao housegirl alafu mlete HOUSEBOY nyumbani.kazi kwisha,kusema kwa mumeo kuna mawili kuaribu au kujenga.
 
huyo ba mkwe inawezekana ameponeshwa na huyo mdogo wako!
 
Back
Top Bottom