motza
Member
- Jun 27, 2012
- 7
- 3
Nimemaliza kidato cha nne hapo mwaka jana.
Ninapenda sana kuchukua PCM, But kwa uelewa wangu mdogo na maoni ya baadhi ya watu inasemekana kwamba PCM Haina ajira serikalini unless kwenye makampuni binafsi (ambako kuna nepotism)... Kama kuna ajira zaidi ya hizo nijulishe tafadhali.
HILI LINANIKATISHA TAMAA SANA NA KUNIFANYA NIHISI KWAMBA NIKISOMA PCM SIPATI AJIRA TOFAUTI NA UALIMU.
Kwa upande wa PCB, INASEMEKANA kuwa kuna ajira za moja kwa moja serikalini ama kwa kujiajili mwenyewe. Na mimi ninasoma ili nipate ajira niweze kujitegemea.
MAONI YAKO NDIYO YATAKAYONIFANYA NIWE NA MAAMUZI MAZURI.
Natanguliza shukrani zangu kwa mtakao nishauri...
Karibuni kwa ushauri....
Ajira zenyewe za serikalini unazodhani utapata ni za kisenge. Soma kozi unayoipenda na kuiweza. As long as unaiweza na utafaulu vizuri, ajira au kujiajiri kutakuja baadae.
Mi binafsi ni engineer. Nlichagua njia hii tangu form one. Advance nilichaguliwa kusoma PCB, nikakomaa kubadilisha kwenda PCM ingawa watu walinipa porojo kama hizo unazoambiwa kuhusu ajira. Nimeajiriwa na natengeneza millions (za kitanzania), na nina mpango wa kuachana na ajira na kuanza kufanya mambo yangu binafsi.