Nichukue uamuzi gani kisheria

STREET SMART

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
837
Reaction score
672
Kwa kifupi.....Kuna family friend ambaye nilimjua kutokana na yeye kufahamiana na wazazi wangu, huyu jamaa anaishi kwenye wilaya moja za mkoa wa Mtwara ambapo pia ndipo nyumbani kwetu kwa wazazi wangu. Nilizoeana na huyu jamaa nikawa nikienda huko napita kwake tunapiga stori mbili tatu naondoka. Mwaka wa juzi alinitafuta kwenye simu akaniambia kuwa amepata tenda ya kuwapa chakula na makazi (jamaa anamiliki gesti moja) watu wanaokimbiza mwenge wa uhuru na kuwa amepungukiwa kiasi cha milioni mbili. Aliniomba nimkopeshe kiasi hicho cha pesa kwa kuandikishana kwa mtendaji wa kata.....kutokana na mimi kuwa naishi dar es salaam nilikubaliana naye kuwa ntamkopesha pesa (2,000,000) hizo anirudishie baada ya mwezi mmoja shilingi 2,500,000 (kiasi atakachorudisha alikitaja yeye mwenyewe), na pia nilikubaliana naye kuwa ataandikishana na mdogo wangu ambaye yupo kule na wanafahamiana pia.

Nilimkopesha na waliandikishiana na mdogo wangu kama tulivyokubaliana. Baada ya mwezi mmoja huyu jamaa akaanza kunizungusha kuwa hajalipwa na Halmashauri ambayo ndio ilishugulikia mbio za mwenge, Tulikorofishana sana kwenye simu na baada ya meizi kama minne alinitumia milioni moja akiahidi kumaliza deni baada ya muda mfupi.

Ukaisha mwaka mzima akiwa hajalipa pesa yoyote zaidi, huku akijitetea kuwa amewafungulia Halmashauri kesi ya madai kwenye Mahakama ya wilaya. Ikapita miezi sita zaidi na sasa akawa hapokei simu yangu wala hajibu meseji zangu. Nikaamua kufunga safari kumfatilia, aliposikia kuwa nimeenda kesho yake alfajiri akasafiri kwenda Dar es salaam, Nikaenda kufatilia Mahakani kama kweli anamadai au kesi yoyote na pia nikafatilia Halmashauri kama kuna madai yake yoyote - Huko kote niligundua kuwa nimetapeliwa kwani hakuna madai yoyote wala pesa yoyote anayodai. Nikafungua shauri mahakani lakini tapeli wangu kila akipelekewa samansi kuitwa anajificha au hapokei na akijua nipo kule atasafiri kwenda kujificha sehemu.

Nilikuwa naomba nisaidiwe mawazo ya kisheria ktk hili swala, Je naweza kumkamata mkewe ambaye anamsaidia kumficha? pili katika kuandikishana aliweka ofa ya makazi kama dhamani ya huo mkopo sheria inaniruhusu vipi kuitumia hii OFA kupata haki yangu.

Sasa ni zaidi ya mwaka umepita hapokei simu yangu wala hajibu meseji zangu hata nikibadilisha namba. Msaada wenu wa mawazo unahitajika wakuu.
 
Swali
Walipoandikishana na mdogo wako, walitumia majina yako au ya mdogo wako?
2. Je, kiasi kilichoandikwa kukopwa ni 1 million au 1.5milioni (let away payable and receivable amount)
3.summons ilikuwa inapelekwa kwa mtindo upi?

Nipe ufahamu wako juu ya hayo tushauriane cha kufanya!
 

1. waliandikishana na mdogo wangu kwa majina yao, ila aliweka kwa niaba yangu. yani namkopesha fulani kwa niaba ya kaka yake ambaye ndo mimi
2.Mkataba unasema alikopa shilingi milioni mbili na atarudisha shilingi milioni mbili na nusu kwa tarehe iliyoandikwa kwenye mkataba
3. Samansi alipewa mdogoangu nikaongozana naye mpaka kwa mjumbe wake (tapeli) wa nyumba kumi ....mjumbe akakataa kuipokea kumpelekea kwa madai ya kwamba familia ya mjumbe na familia ya tapeli zina ugomvi hawaongeleshani, na mjumbe akaongea zaidi kuwa amechoshwa na watu wanaokuja kumshtakia tapeli kwa dhuluma anazofanya.
4.Tukibahatika kumkuta mkewe kumkabidhi samansi anakataa kupokea kwa maelezo yeye hajausishwa kwenye kukopeshana.
 
Mmmh!!!! watu wengine, sasa mjumbe anakataaje kupokea barua wakati huo ni wajibu wake?????????

Viongozi wa Tanzania hawajielewi kabisa, ugomvi binafsi hauhusiani na majukumu ya kazi hata kidogo.
 
Mmmh!!!! watu wengine, sasa mjumbe anakataaje kupokea barua wakati huo ni wajibu wake?????????

Viongozi wa Tanzania hawajielewi kabisa, ugomvi binafsi hauhusiani na majukumu ya kazi hata kidogo.

Kichwa kikioza miguu haiwez kuwa mizima. viongozi wa juu uozo mtupu
 
Makosa yaliyofanyika kwenye huo mkataba unakufunga mwenyewe tena ni kesi rahisi sana ingekuwa mm ndio mdaiwa!
1:Mkataba umeandikwa kwamba jamaa amekopa 2m na atalipa 2.5m,swali Je?ww unataasisi ya kukopesha watu iliyosajiliwa na serikali hadi ukopeshe mtu kwa Riba?
2:Je huo mkataba ulipelekwa mahakamani kabla ya makabidhiano ya pesa ili kutambulika kisheria?
3:Bado namba 1 inakufunga
Ushauri wa bure ni hv unapomkopesha mtu mfano 2m,inabidi muandikishane kuwa umemkopesha 2.5m badala yakusema ulimkopesha 2m ili alipe 2.5m,pili hakikisha kwamba mkataba wenu unatambulika mahakamani kabla hamjakabiziana pesa na Logoff
 
Haki ya mtu haipotei, unamambo mawili ya kufanya, kwanza mfungulie kesi ya madai kudai kiasi kile ulichomkopesha, nakwakuwa yeye anajifanya mjanja, hata km alikurudishia mili 1 kama hakumuandikishiana, wewe kadai zote mil 2.

Njia yapili nenda kituo cha polisi kamfungulie kesi ya jinai ya kujipatia fedha KWA njia ya udanganyifu, kwani alikudanganya kuwa anagest na kapata tenda, pili akakudanganya kuwa hawajamlipa, tatu akakudanganya kuwa atakuongezea laki tano, tatu akakudanganya kuwa amefungua kesi akidai. Huo ni udanganyifu na ulikushawishi uweze kutoa hiyo Pesa.

I submit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…