STREET SMART
JF-Expert Member
- Feb 19, 2010
- 837
- 672
Kwa kifupi.....Kuna family friend ambaye nilimjua kutokana na yeye kufahamiana na wazazi wangu, huyu jamaa anaishi kwenye wilaya moja za mkoa wa Mtwara ambapo pia ndipo nyumbani kwetu kwa wazazi wangu. Nilizoeana na huyu jamaa nikawa nikienda huko napita kwake tunapiga stori mbili tatu naondoka. Mwaka wa juzi alinitafuta kwenye simu akaniambia kuwa amepata tenda ya kuwapa chakula na makazi (jamaa anamiliki gesti moja) watu wanaokimbiza mwenge wa uhuru na kuwa amepungukiwa kiasi cha milioni mbili. Aliniomba nimkopeshe kiasi hicho cha pesa kwa kuandikishana kwa mtendaji wa kata.....kutokana na mimi kuwa naishi dar es salaam nilikubaliana naye kuwa ntamkopesha pesa (2,000,000) hizo anirudishie baada ya mwezi mmoja shilingi 2,500,000 (kiasi atakachorudisha alikitaja yeye mwenyewe), na pia nilikubaliana naye kuwa ataandikishana na mdogo wangu ambaye yupo kule na wanafahamiana pia.
Nilimkopesha na waliandikishiana na mdogo wangu kama tulivyokubaliana. Baada ya mwezi mmoja huyu jamaa akaanza kunizungusha kuwa hajalipwa na Halmashauri ambayo ndio ilishugulikia mbio za mwenge, Tulikorofishana sana kwenye simu na baada ya meizi kama minne alinitumia milioni moja akiahidi kumaliza deni baada ya muda mfupi.
Ukaisha mwaka mzima akiwa hajalipa pesa yoyote zaidi, huku akijitetea kuwa amewafungulia Halmashauri kesi ya madai kwenye Mahakama ya wilaya. Ikapita miezi sita zaidi na sasa akawa hapokei simu yangu wala hajibu meseji zangu. Nikaamua kufunga safari kumfatilia, aliposikia kuwa nimeenda kesho yake alfajiri akasafiri kwenda Dar es salaam, Nikaenda kufatilia Mahakani kama kweli anamadai au kesi yoyote na pia nikafatilia Halmashauri kama kuna madai yake yoyote - Huko kote niligundua kuwa nimetapeliwa kwani hakuna madai yoyote wala pesa yoyote anayodai. Nikafungua shauri mahakani lakini tapeli wangu kila akipelekewa samansi kuitwa anajificha au hapokei na akijua nipo kule atasafiri kwenda kujificha sehemu.
Nilikuwa naomba nisaidiwe mawazo ya kisheria ktk hili swala, Je naweza kumkamata mkewe ambaye anamsaidia kumficha? pili katika kuandikishana aliweka ofa ya makazi kama dhamani ya huo mkopo sheria inaniruhusu vipi kuitumia hii OFA kupata haki yangu.
Sasa ni zaidi ya mwaka umepita hapokei simu yangu wala hajibu meseji zangu hata nikibadilisha namba. Msaada wenu wa mawazo unahitajika wakuu.