Nick wa Pili na mbwembwe za usomi

dawa yenu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
2,825
Reaction score
3,675
Leo imenipendeza kumzungumzia huyu mkali wa "kunata na biti!" Kumbuka sio kila mwenye uwezo wa kunata na biti ni mwanamuziki mzuri. Huyu ni msomi, tena miongoni mwa wasanii wachache sana waliobahatika kubukua vitabu (kumbuka kwa elimu ya Tanzania kusoma sio kigezo cha kuelimika). jamaa anatokea Arusha akiwakilisha kundi la WEUSI. ameweza kuhimili mikiki ya industry kwa zaidi za miaka kumi sasa tokea enzi zile za "NIAJE NI VIPI?" halafu akatisha sana kwenye ile ngoma ya "UJAMAA" bonge moja la collaboration akiwa na Pipi wa THT then hapa kati kati akaachia mapini mengi sana heavy na hapa juzi juzi aka "switch" akasema anataka 'kucum" hapa alikuwa na wenzake ila kabla ya hapo walisema wanataka "kuliamsha dude" yeaah wenyewe wanakuambia wame "switch"

Kwanini namzungumzia Nick wa pili?
Jamaa kafanikiwa kujinasibisha na usomi. Na amekuwa akichagiza kwa kuibua hoja kadha wa kadha huko twitter na instagram. Hapo ndipo ninapotaka nipadadavue leo. Jamaa kafanikiwa sana kuuaminisha umma kuwa yeye ni msomi na mwenye mawazo ya kiwango cha juu sana labda mfano wa akina Jenerali Ulimwengu au Issa Shivji. Kwanza kabisa hii ni violance maana anawafanya watu wawe inferior kwake watazame hoja zake kwa jicho lililojaa wenge na kushindwa kuchambua hoja hizo vizuri. Jmaa sio mzuri wa kujenga hoja ila yuko vizuri kwenye kucheza cheza na maneno na kuyarudia rudia hatimaye hata hoja dhaifu inaonekana tata, kumbe utata upo kwenye lugha ila sio maudhui ya hoja husika (kasikilize SWEET MANGI utaona hii kitu)

Ukiitazama hoja yoyote ya Nick as whole lazima ikuchanganye na utaishia kuvurugwa. Hoja ya Nick kwanza ivunje vunje katika parts ndogo ndogo kisha idadavue utaona maajabu yaani hakuna lolote. sasa Nick aache kutumia ujanja ujanja ambao unapelekea watu kushindwa kutambua msingi wa hoja zake ila aweke hoja vizuri ieleweke kisha ijadiliwe na kila mtu. yaani kuwa complicated sio kigezo cha usomi. Nick ajitafakari upya.

ni hayo tu.....
 

Attachments

  • nick wa pili.jpg
    27.4 KB · Views: 84
Sina shida na Nick Ila kuna kashikaji kake na Nick kanaitwa Hassan Ngima ka kule mawingu TV yaani kajamaa kanajifanya kanajua kila kitu cha Duniani afu kwa kutegemea uteuzi kanapenda sana kumfagilia mzee baba na chama kongwe!! Daah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…