NIDA inatarajia kuanzisha vitambulisho vya Taifa vya Smartcard

Nida hawa hawa wa Tanzania au kuna nida wengine kutoka nchi wahisani acha tusubiri tuone.
 
Mfumo mmoja tu umewatoa jasho mpaka leo ID za kitaifa hazitoshi,wataweza kuifanya mifumo yote isomane,benk,leseni nk?kama kuipata leseni tu na passport ni mbinde kama vile unamtafuta raia mwenye asili ya kigogo Ukraine!!hapa naona mradi wa upigaji kwa mbaaaali.
 
Zanzibar alianzisha vitambulisho vya mzanzibari na wakaafanikiwa sanaa, Kama kawaida zao wazee wa chuki wakaanzisha vyao mpaka leo sijui mwaka wa ngapi zoezi limewashinda njiani😂😂😂.
 
Kitengo cha passport ndio kinatakiwa ku intergrate na NIDA, sababa NIDA tayari anayo hiyo service

Hapa naweza mtetea NIDA, ila tatizo ni bei za NIDA kwa kila verification ni kubwa baadhi ya taasisis ndogo na makampuni madogo hawaziwezi
 
Njaa tupu wala rushwa wakubwa hawa, pale ni kujuana na rushwa tuu ndio utapata ID la sivyo subiri mpaka yesu arudi
 
Kuhalalisha upigaji tu, hili halijaisha washadakia lingine.
 
Wanatengeneza mlo tu
Hizo hela wanazotaka wajengee vyoo
Rubbish
 
Hapa naweza mtetea NIDA, tatizo ni bei za NIDA kwa kila verification ni kubwa baadhi ya taasisis ndogo na makampuni madogo hawaziwezi
Hujaeleweka fafanua
 
Wanatengeneza mlo tu
Hizo hela wanazotaka wajengee vyoo
Rubbish
Hakuna mtu anazuia mtu kula.Wale ila wafanye kazi ya kuonekana hasa kila mwananchi aone
Hilo eneo la integration walifanye upesi kuunga idara zote muhimu zinazohudumia wananchi zinazohitaji utambulisho
 
Sawa.
 
NIDA wajitokeze watuambie ni sheria ipi itamlinda mwananchi dhidi ya matumizi mabaya ya taarifa zake??
 
Hapo walikuwa wanampa nani taarifa kwa Kingereza!?
 
Ninatumaini hii itawasaidia Mamlaka ya kutoa passport kuacha kudai umlete aliyeshuhudia baba yako akizaliwa - wakati wewe mwombaji una miaka 60!
😂🤣 Kuna rafiki yangu yeye alijaza kwamba yeye mwenyewe alimshuhudia baba yake kuzaliwa. Baba yake alishafariki miaka 10 myuma. Wakakubali na kuprocess passport yake.
 
😂🤣 Kuna rafiki yangu yeye alijaza kwamba yeye mwenyewe alimshuhudia baba yake kuzaliwa. Baba yake alishafariki miaka 10 myuma. Wakakubali na kuprocess passport yake.
Hadithi hiyo alikufundisha nani
 
NIDA wajitokeze watuambie ni sheria ipi itamlinda mwananchi dhidi ya matumizi mabaya ya taarifa zake??
Wajieleze kivipi wakati wewe ndie utaenda kuzitaka mfano unataka jisajili line ya simu unawapa kitambulisho champ cha NIDA na dole lako gumba ndipo zinakuja

Zinakuja on demand ya kwako mwenyewe

Usipoweka hilo dole lako haziji hana uwezo wa kuzivuta

Wewe ndie labda ujieleze kwa kumpa kitambulisho cha NIDA msajili laini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…