NIDA inawasaidiaje watu waliohama maeneo waliyoombea vitambulisho?

NIDA inawasaidiaje watu waliohama maeneo waliyoombea vitambulisho?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kama mtu aliomba kitambulisho chake akiwa Kigoma halafu akahamia Dar es Salaam atafanye kupata kitambulisho chake kutoka Kigoma?
20250118_092019.jpg
 
Kama mtu aliomba kitambulisho chake akiwa Kigoma halafu akahamia Dar es Salaam atafanye kupata kitambulisho chake kutoka Kigoma?
View attachment 3205022

Hiinkuomba kusaidiwa ni kulea majipu yaliyoota na kumea kipindi cha mwamba.

Hii ni awamu mpya ya Lissu:

"Dawa ni kumwaga mboga, wabaki navyo tuone ugali wataula je!"
 
NIDA wapeleke vitambulisho kwenye ofisi zao waliko wenye vitambulisho. kama wanaona hilo zoezi ni gumu warefushe muda hata miezi mitatatu watu wafuate vitambulisho vyao huko mbali walikojiandikisha.
 
NIDA wapeleke vitambulisho kwenye ofisi zao waliko wenye vitambulisho. kama wanaona hilo zoezi ni gumu warefushe muda hata miezi mitatatu watu wafuate vitambulisho vyao huko mbali walikojiandikisha.
Mtu yuko Dar atumie laki mbili siku 3 kufuata kitambulisho Kigoma?
 
Wanaposema wenye vitambulisho wanakaidi kuchukua vitambulisho vyao si kweli. Wanashitukiza wananchi kwamba watasitisha matumizi ya namba za vitambulisho kwamba watafuta mtu aanze upya kujiandikisha apate kingine au ni mpaka ujitokeze kwenda kuchukua ndio hiyo namba iachiwe? Ishu ni kwamba wananchi wako mbali na mikoa walikojiandikisha, watoe date line ndefu wananchi wapange safari kwenda mikoa walikojiandikisha kama wanaona kuwapelekea waliko ni zoezi gumu. Mawasiliano yapo ila wanafanya kazi kizamani sana
 
NIDA wanatakiwa kuendana na teknolojia ya sasa. Hicho kitambulisho iwe rahisi mtu kukipata popote mkoani alipo. Ni kukopi data tu mtu anapata kitambulisho chake alipo kama kusafirisha ni ngumu, mitambo wanayo na tayari data wanazo, ni kuhamisha tu kwenye gamba jingine huko kwenye ofisi zao za mikoani
 
Back
Top Bottom