Mimi kama mtanzania mzalendo nasikitishwa sana na taasi za umma ambazo zinatumia fedha za umma katika kazi zinazotekelezwa kwa viwango vya chini hatimaye kutumia fedha nyingi za wananchi katika jambo moja mara kwa mara wakati pesa inayopotea ingeweza kufanikisha utekelezaji wa masuala ya msingi yanayolikabili taifa.
Moja ya taasisi inayonichosha katika hili ni Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA). Mfano nikiwa mkoani Mbeya nilijiandikisha kwa ajili ya kupata kitambulisho cha uraia, ambapo nilifanikiwa kupata namba lakini kitambulisho sikukipata mpaka nikahamia mkoa mwingine.
Nikiwa mkoa mwingine nilitembelea tovuti ya NIDA kuona kama kitambulisho changu kipo tayari na nikabaini kilikuwa tayari. Niliagiza mtu wangu wa karibu akanichukulie kutokana na NIDA kuruhusu watu kuchukuliana lakini alipofika akaambiwa kimerudishwa ofisi za NIDA mkoani.
Basi siku moja mwezi Desemba 2025 nilipata nafasi ya kutembelea Mbeya nikaona iwe fursa pia ya kwenda kuchukua kitambulisho changu lakini cha kushangaza nilipofika nikaambiwa kitambulisho hakipo itakuwa kimefutika, kimerudishwa kuprintiwa upya.
Sasa nawauliza NIDA ni material gani wanatumia kuprint vitambulisho hivyo kiasi cha kufutika kabla ya kumfikia mwananchi? Je, huu si uchakachuaji?
Hayo material mliyotumia hamkujua kama vitambulisho kabla ya matumizi? Au mlifanya makusudi ili kupata pa kupigia kodi zetu raia?
Je, ni vitambulisho vingapi vimefutika kabla hata ya kuwafikia wahusika? Kwamba hakuna material imara ya kufanya kitambulisho kidumu muda mrefu? Mimi kama mtanzania naona hapa kuna kupigwa kabisa.