SI KWELI NIDA na RITA wametoa mkataba kwa shirika la Babu leo LTD kufanya marekebisho ya majina kwenye vyeti

SI KWELI NIDA na RITA wametoa mkataba kwa shirika la Babu leo LTD kufanya marekebisho ya majina kwenye vyeti

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu

Nimekutana na hii barua ambayo inasema NIDA na RITA wametoa mkataba kwa shirika la Babu leo LTD kufanya marekebisho ya majina kwenye vyeti? kuna ukweli wa hizi taarifa?
Xy.jpg
XYR.jpg
XYZ.jpg
 
Tunachokijua
NIDA na RITA ni mamlaka za serikali zilizoanzishwa kisheria zikiwa na majukumu tofauti. NIDA ikijihusisha na vitambulisho vya taifa wakati RITA ikijihusisha na huduma za ufilisi, usajili wa vizazi na vifo.

kupitia mtandao wa Facebook mtumiaji mmoja alichapisha taarifa inayoeleza kuwa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa kushirikiana na chombo cha utoaji wa huduma za usajili, ufilusi na udhamini (RITA) wanafanya marekebisho ya majina kwenye vyeti vya kuzaluwa kwa wanafunzi wa ngazi zote kwa kushirikiana na shirika la Babuleo LTD.

JamiiCheck imefuatilia tangazo hilo na kujiridhisha kuwa lina lengo la ulaghai kwa wananchi.

Tangazo hilo linadai kuwa taasisi hizo mbili za serikali yaani NIDA na RITA zinashirikiana na taasisi ya Babuleo Ltd si kweli kwani taasisi hizo zinafanya majukumu yake kwa kujitegemea na hawajawahi kutangaza kushirikiana na taasisi yenye jina la Babuleo.

Gharama zilizoainishea kwenye tangazo hilo si halisi kwani kwa mujibu wa RITA kubadilisha jina kwenye cheti ni Tsh. 13,000 wakati kwa upande wa NIDA ni Tsh. 20,000 tofauti na bei za kwenye tangazo hilo ambazo ni 35,850 kwa NIDA na 32,850 kwa RITA.
1758015867727-png.3473274


Tangazo hilo pia lina mapungufu kadhaa ikiwemo makosa ya kiuandishi na aina tofauti ya mwandiko na ile inayotumiwa na matangazo halisi ya mamlaka hizo yaani NIDA na RITA.

Aidha tangazo hilo halijatolewa wala kuchapishwa katika kurasa rasmi za NIDA na RITA
Back
Top Bottom