NIDA: Ruksa kubadili Vitambulisho vilivyoisha muda au vyenye ukomo kwa Tsh. 20,000

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) imesema ni ruksa kwa yeyote anayetaka kubadilisha kitambulisho chake cha Taifa kwa kulipia gharama ya Sh20,000.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Geoffrey Tengeneza ameyasema hayo Jumatano Februari 22, 2023 wakati wa mjadala ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kupitia mtandao wa kijamii ya Twitter (Mwananchi Twitter Space) kujadili uamuzi wa kuondoa ukomo wa muda kwenye vitambulisho vya Taifa.

“Mwananchi yeyote anaweza kwa hiari yake kuomba kitambulisho kipya kisicho na ukomo wa muda; lakini anayeamua kufanya hivyo awe tayari kulipia gharama ya Sh20, 000,” amesema Tengeneza.

Amesema mwenye nia hiyo atalazimika kufika kwenye ofisi yoyote ya Nida iliyo jirani kukamilisha taratibu ikiwemo kuongeza taarifa mpya zisizokuwepo kwenye kitambulisho chake cha awali.

Wakijadili mada inayosema “Vitambulisho vya Taifa kuondolewa ukomo kuna athari gani?” Wadau wamegawanyika katika makundi mawili, moja likunga mkono mpango huo wa Serikali na lingine likipinga.

Wanaounga mkono akiwemo mbunge wa zamani, Suzan Lyimo, wanasema mpango huo utawaondolea wananchi adha ya kulazimika kutafuta vitambulisho vipya kila ukomo wa muda unapofika huku wakitumia muda mrefu kutafuta vitambulisho badala ya kushiriki shughuli za uzalishaji.

“Hakukuwa na sababu za kuweka ukomo kwenye vitambulisho vya Taifa kwa sababu uraia ni suala lisilo na ukomo wa muda,” amesema Suzan Lyimo, mbunge wa zamani wa Viti Maalum (Chadema) ambaye kwa sasa anatambulishwa na chama chake kama Spika wa Bunge la Wananchi.

Akichokoza mada wakati wa mjadala huo, William Shao amesema uamuzi huo una faida chanya na hasi kwa wananchi na Serikali yenyewe huku akitaja faida kuwa ni fursa ya kuingiza taarifa mpya kulingana na anuani ya makazi, umri, picha na mabadiliko ya teknolojia.

Amesema japo yapo mataifa mengi duniani yakiwemo ya Kiafrika kama Kenya, Botswana na Ghana vinatoa vitambulisho vya kudumu vya Taifa, suala la kuisha vitambulisho ni muhimu ili kuingiza taarifa mpya kuanzia mabadiliko ya imani za kidini, ndoa, kiwango cha elimu, mabadiliko ya makazi na uraia.

Pia Soma:
- NIDA: Ruksa kubadili Vitambulisho vilivyoisha muda au vyenye ukomo kwa Tsh. 20,000

MWANANCHI
 
Ehe kwa hiyo wakilipia mnawapa namba tu huku ,kitambulisho halisi
Hamtoi

Ova
 
mabadiliko ya imani za kidini, ndoa, kiwango cha elimu, mabadiliko ya makazi na uraia.
Dini kwenye vitambulisho?

Kiwango cha elimu so what? Kwani certificate zina kazi gani.

Makazi mtu atakuwa anaprinti vitambulisho kila anapohama mta
 
Dini kwenye vitambulisho!!?
Kiwango cha elimu so what? Kwani certificate zina kazi gani
Makazi mtu atakuwa anaprinti vitambulisho kila anapohama mta
Kuna wanao penda kufanya hivyo

Lile dodoso lina maswali yote

Hali ya ndoa
Dini
Unapo ishi/anuani ya makazi
Majina yako
Elimu yako
Nk

Sasa vingi vina weza badilika kulingana na wakati, mfano picha yako...

Kwa namna hii tuna omba hati za kusafiria ziige huu utaratibu, ukomo uwe pale kitabu kinapo jaa tu
 
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) imesema ni ruksa kwa yeyote anayetaka kubadilisha kitambulisho chake cha Taifa kwa kulipia gharama ya Sh20,000.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Geoffrey Tengeneza ameyasema hayo Jumatano Februari 22, 2023 wakati wa mjadala ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kupitia mtandao wa kijamii ya Twitter (Mwananchi Twitter Space) kujadili uamuzi wa kuondoa ukomo wa muda kwenye vitambulisho vya Taifa.

“Mwananchi yeyote anaweza kwa hiari yake kuomba kitambulisho kipya kisicho na ukomo wa muda; lakini anayeamua kufanya hivyo awe tayari kulipia gharama ya Sh20, 000,” amesema Tengeneza.

Amesema mwenye nia hiyo atalazimika kufika kwenye ofisi yoyote ya Nida iliyo jirani kukamilisha taratibu ikiwemo kuongeza taarifa mpya zisizokuwepo kwenye kitambulisho chake cha awali.

Wakijadili mada inayosema “Vitambulisho vya Taifa kuondolewa ukomo kuna athari gani?” Wadau wamegawanyika katika makundi mawili, moja likunga mkono mpango huo wa Serikali na lingine likipinga.

Wanaounga mkono akiwemo mbunge wa zamani, Suzan Lyimo, wanasema mpango huo utawaondolea wananchi adha ya kulazimika kutafuta vitambulisho vipya kila ukomo wa muda unapofika huku wakitumia muda mrefu kutafuta vitambulisho badala ya kushiriki shughuli za uzalishaji.

“Hakukuwa na sababu za kuweka ukomo kwenye vitambulisho vya Taifa kwa sababu uraia ni suala lisilo na ukomo wa muda,” amesema Suzan Lyimo, mbunge wa zamani wa Viti Maalum (Chadema) ambaye kwa sasa anatambulishwa na chama chake kama Spika wa Bunge la Wananchi.

Akichokoza mada wakati wa mjadala huo, William Shao amesema uamuzi huo una faida chanya na hasi kwa wananchi na Serikali yenyewe huku akitaja faida kuwa ni fursa ya kuingiza taarifa mpya kulingana na anuani ya makazi, umri, picha na mabadiliko ya teknolojia.

Amesema japo yapo mataifa mengi duniani yakiwemo ya Kiafrika kama Kenya, Botswana na Ghana vinatoa vitambulisho vya kudumu vya Taifa, suala la kuisha vitambulisho ni muhimu ili kuingiza taarifa mpya kuanzia mabadiliko ya imani za kidini, ndoa, kiwango cha elimu, mabadiliko ya makazi na uraia.

Pia Soma:
- NIDA: Ruksa kubadili Vitambulisho vilivyoisha muda au vyenye ukomo kwa Tsh. 20,000

MWANANCHI
wametafuta mlango wa kukusanya mapato mpaka wameupata.. haya sasa kazi kwenu
 
Hamjatupa vitambulisho toka mwaka juzi leo hii mnapiga mchakato wa elfu 20
 
Kwa namna hii tuna omba hati za kusafiria ziige huu utaratibu, ukomo uwe pale kitabu kinapo jaa tu
Siku hizi hawatumii kitabu wanasema za vitabu zimeshafutwa zipo za biometric
 
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) imesema ni ruksa kwa yeyote anayetaka kubadilisha kitambulisho chake cha Taifa kwa kulipia gharama ya Sh20,000.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Geoffrey Tengeneza ameyasema hayo Jumatano Februari 22, 2023 wakati wa mjadala ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kupitia mtandao wa kijamii ya Twitter (Mwananchi Twitter Space) kujadili uamuzi wa kuondoa ukomo wa muda kwenye vitambulisho vya Taifa.

“Mwananchi yeyote anaweza kwa hiari yake kuomba kitambulisho kipya kisicho na ukomo wa muda; lakini anayeamua kufanya hivyo awe tayari kulipia gharama ya Sh20, 000,” amesema Tengeneza.

Amesema mwenye nia hiyo atalazimika kufika kwenye ofisi yoyote ya Nida iliyo jirani kukamilisha taratibu ikiwemo kuongeza taarifa mpya zisizokuwepo kwenye kitambulisho chake cha awali.

Wakijadili mada inayosema “Vitambulisho vya Taifa kuondolewa ukomo kuna athari gani?” Wadau wamegawanyika katika makundi mawili, moja likunga mkono mpango huo wa Serikali na lingine likipinga.

Wanaounga mkono akiwemo mbunge wa zamani, Suzan Lyimo, wanasema mpango huo utawaondolea wananchi adha ya kulazimika kutafuta vitambulisho vipya kila ukomo wa muda unapofika huku wakitumia muda mrefu kutafuta vitambulisho badala ya kushiriki shughuli za uzalishaji.

“Hakukuwa na sababu za kuweka ukomo kwenye vitambulisho vya Taifa kwa sababu uraia ni suala lisilo na ukomo wa muda,” amesema Suzan Lyimo, mbunge wa zamani wa Viti Maalum (Chadema) ambaye kwa sasa anatambulishwa na chama chake kama Spika wa Bunge la Wananchi.

Akichokoza mada wakati wa mjadala huo, William Shao amesema uamuzi huo una faida chanya na hasi kwa wananchi na Serikali yenyewe huku akitaja faida kuwa ni fursa ya kuingiza taarifa mpya kulingana na anuani ya makazi, umri, picha na mabadiliko ya teknolojia.

Amesema japo yapo mataifa mengi duniani yakiwemo ya Kiafrika kama Kenya, Botswana na Ghana vinatoa vitambulisho vya kudumu vya Taifa, suala la kuisha vitambulisho ni muhimu ili kuingiza taarifa mpya kuanzia mabadiliko ya imani za kidini, ndoa, kiwango cha elimu, mabadiliko ya makazi na uraia.

Pia Soma:
- NIDA: Ruksa kubadili Vitambulisho vilivyoisha muda au vyenye ukomo kwa Tsh. 20,000

MWANANCHI
Vitambulisho hivyo vinatoka baada ya miaka mingapi ukishaomba?
 
S

Asante
 
NIDA ni jipu. Tokea 2019 hadi leo sijapata kitambulisho. Mwaka jana nilifuatilia nikakutana na majibu yasiyoridhisha.

Niliambiwa nitatumiwa message. Kuweni serious NIDA. Huu ni mwaka wa tano unaenda. Hata Uhamiaji wamewapiga bao, Passport ya kusafiria unaipata ndani ya siku saba za kazi.

NIDA ni wababaishaji tu. At least mngeweka hata mfumo wa online wa kuangalia kama kitambulisho kimetoka na sehemu ya kukipata. Wapo tulijiandikisha tukiwa Dodoma kwa sasa tupo Butiama.

NIDA ifumuliwe. Haina ufanisi wala ubunifu. Ni mizigo.
 
Back
Top Bottom