NIDA wamenijibu kuwa hawana mpango wa kutoa vitambulisho vya Utaifa tena

NIDA wamenijibu kuwa hawana mpango wa kutoa vitambulisho vya Utaifa tena

Kwakweli nida nikeerooo mpaka mboso kawaimbia ndokwaaanza tunajidaaiiii Kama afisa waniiida hahaaaa
Hili suala la vitambulisho vya taifa limekuwa kero sana. Kuna watu wengi wamejiandikisha toka 2017 ila mpaka sasa hawana vitambulisho.

Leo nimeenda kufuatilia kitambulisho changu nilichojiandikisha 2018 na hayo ndio majibu niliyopewa.

Kuna kitu gani kipo NIDA? Mbona viongozi wako kimya huku NIDA wakiendelea kutuvimbia wananchi?
 
Mi nilifuatilia pale kawe mpaka nikakata tamaa.

Cha kura utakipata hapo hapo.
 
Mkono mtupu haulambwi wale jamaa wananjaa sana ukiwawekea chambo tu ndani ya siku tatu tu unapata kitambulisho.
 
Ilihali taasisi nyingi hazipokei number ya Nida bila kitambuisho kamili...
 
Vitambulisho vinaendelea kutolewa kama kawaida katika ofisi zote za usajili za Wilaya nchini. Lakini pia vilivyopelekwa katika ofisi za watendaji wa vijiji na Serikali za Mitaa vinatolewaNi ofisi ya Wilaya gani hiyo uliyoenda Mkuu ukaambiwa hawatoi tena? labda kama walikuambia kuwa hakijachapishwa au hakijawafikia hapo ofisini ili kukitoa kwako kama mhusika hapo sawa. Lakini si kwamba hakuna mpango wa kutoa Vitambulisho vya Taifa tena , hiyo si kweli. Yawezekana aliyekujibu hakuwa mtumishi.
Ofisi ya Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha
 
Back
Top Bottom