BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) imeanza kuchapa upya vitambulisho vilivyochapishwa chini ya kiwango, hivyo imewataka wenye navyo kuviwasilisha katika ofisi zake zilizo karibu nao vichapwe upya.
Hayo yamesemwa leo Alhamisi Julai 4, 2024 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Nida, Geofrey Tengeneza alipozungumza na Mwananchi.
Amesema hatua hiyo imetokana na malalamiko kutoka kwa wananchi wa mikoa mbalimbali kuhusu ubora hafifu wa baadhi ya vitambulisho hivyo.
"Tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro Dar es Salaam na mingine, kuwa vitambulisho walivyopewa vimefutika picha na majina," amesema.
Baada ya kufanya utafiti na kubaini ukweli juu ya changamoto hiyo na Nida imeamua kuvikusanya kutoka kwa wananchi ili kuvichapisha upya.
"Napenda kuchukua nafasi hii kuujulisha umma wa Watanzania kwamba yoyote mwenye kitambulisho kilichofutika picha na maandishi akirejeshe kwenye ofisi za kata yake, au ofisi za Nida zilizopo karibu naye ili achapiwe kipya ndani ya muda mfupi," amesema.
MWANANCHI
Pia Soma:NIDA: Ruksa kubadili Vitambulisho vilivyoisha muda au vyenye ukomo kwa Tsh. 20,000