Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuelezea changamoto zinazojitokeza kwenye mchakato wa Wananchi kujiandikisha kwa ajili ya kupata Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora, ufafanuzi umetolewa na Mamlaka hiyo.
Awali mdau alilalamikia changamoto ya foleni kubwa, msongamano, fomu kuuzwa na kushauri siku za kufanya zoezi hilo ziongezwe.
Kusoma zaidi hoja za Wadau, bofya hapa:
~ Mwitikio wa wanaojiandikisha NIDA Wilaya ya Uyui ni mkubwa lakini Watendaji na Vifaa havitoshi
~ Waliofanya Uandikishaji Vitambulivyo vya NIDA, Nsololo - Uyui hawajakamilisha kazi, bado watu wengi hawajakamilisha mchakato
Huyu hapa Msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Geofrey Tengeneza anajibu:
FOMU ZA KUJIANDIKISHA NI BURE
Kama kuna mtu anaambiwa atoe hela ili apewe fomu sio sawa, isije kuwa kuna matapeli wanatumia mwanya huo kuwalaghai Watu, kama wapo hao anatakiwa kuripotiwa na kuchukuliwa hatua za Kisheria.
Ikiwa kuna mtu anafanya hivyo, NIDA tunatoa wito Wananchi kumripoti kwa maafisa wetu au kwa Vyombo vya Usalama ili hatua zichukuliwe.
UCHACHE WA WATUMISHI
Ni kweli tuna changamoto ya Watumishi kwa sasa hasa kipindi hiki ambacho kuna zoezi la Watu kwenda kuchukua vitambulisho vyao na wengine kwenda kufanya mchakato wa kujiandikisha.
Tunafanya kugawana ili watu wa pande zote wapate huduma lakini tayari Mamlaka inashughulikia hilo, mfano kwa Mkoa wa Dar es Salaam tumepata Watumishi wapya ambao wameajiriwa kutoka Tume ya Utumishi.
Watumishi hao wapo kwenye mafunzo makao makuu baada ya hapo watasambazwa katika vituo tofauti ili kuongeza nguvu kwenye vituo.
SUALA LA KUONGEZA SIKU LINAJADILIWA
Suala la kuongeza siku kwa Watumishi wetu wanaozunguka katika Kata tumelipokea, tutalijadili kuona kama linawezekana, ikiwa hivyo tutatoa taarifa.
Katika kuonyesha watu wanatakiwa kupata hudumu, maelekezo ni kuwa ofisi hazitakiwi kufungwa saa tis ana nusu babdala yakw wanaendelea hadi saa kumi hadi kumi na moja na wengine hadi zsaa kumi na mbili