Nidhamu mbovu kwa wanafunzi na utoro wa walimu tishio la ubora wa elimu Bagamoyo.

Nidhamu mbovu kwa wanafunzi na utoro wa walimu tishio la ubora wa elimu Bagamoyo.

Happiness2013

New Member
Joined
May 8, 2013
Posts
3
Reaction score
0
Mkurugenzi wa Halmashauri (W) ya Bagamoyo pamoja na wadau wengine wa Wilaya ya Bagamoyo wanakazi kubwa katika kuinusuru elimu ya wilaya ya Bagamoyo ili isishuke.

Kuna sababu nyingi zinazopelekea elimu ya (W ) Bagamoyo kuporomoka. Sababu kubwa ni nidhamu mbovu ya wanafunzi wanaosoma katika shule mbalimbali za wilaya ya Bagamoyo hasa wanafunzi wa shule za sekondari. Wanafunzi hawa wana utovu mkubwa wa nidhamu kwa walimu wao. Vitendo hivi vya utovu wa nidhamu vimekithiri katika shule za sekondari za serikali. Wanafunzi wanadiriki hata kuwapiga walimu na kuwatishia kwa mapanga. Isitoshe kuna baadhi ya wanafunzi wa kike wanajihusisha na vitendo vya umalaya na ukahaba huku wakisahau wajibu wao wa kusoma ili kuandaa maisha yao ya baadae.

Suala la utoro wa walimu nalo ni tatizo kubwa sana katika wilaya ya Bagamoyo. Kuna baadhi ya shule walimu hawafiki kazini mpaka miezi mitatu mpaka mwaka lakini bado wanaendelea kupata mishahara kama kawaida. Walimu hawa wamekuwa wakishirikiana na wakuu wa shule katika uovu huo wa kupokea mshahara bila ya kufanya kazi huku wakiwaacha wanafunzi bila ya kupata haki yao ya kufundishwa.

Jambo la kushangaza shule hizi zilizokithiri kwa utoro wa walimu zipo katika jimbo la waziri wa Elimu ,Dk. Shukuru Kawambwa. Hali hii ya utoro wa walimu imekuwa ikivunja moyo walimu wachapa kazi kwani wanahisi kama wananyonywa, yaani wanakatishwa tamaa na hali ya walimu wenzao wasiofanya kazi lakini wanapokea mshahara kama wanafanya kazi. Walimu hawa wamekuwa chanzo kikubwa cha kushuka kiwango cha elimu katika (W) Bagamoyo kwa vitendo vyao vya utoro uliokithiri.

Serikali ya mkoa wa Pwani imeshindwa kuwawajibisha walimu hawa watoro na wasiofata maadili ya kazi yao badala yake serikali imekuwa ikitumia vibaya pesa za walipa kodi kwa kuwalipa mishahara walimu hawa kana kwamba wanafanya kazi wakati hawafiki kazini.

Baraza la madiwani la (W) Bagamoyo limeshindwa kuwawajibisha walimu hawa wazembe kwa kuhofia kuweka uhusiano mbaya na wakuu wa shule wanaowalinda walimu hawa.

Hivyo kuna haja mamlaka zinazohusika kulivalia njuga suala la nidhamu ya wanafunzi na utoro wa walimu uliokithiri katika wilaya ya Bagamoyo.
 
Wewe subiri ulogwe, si vibaya kwa sababu umetetea maslahi ya raia, Unajua kwa nini wenyewe hawafanyi hivyo unayotoa mdomoni mwako, FUTA haraka uzi wako, unawajuaje wachapakazi wanaofanyakazi, na Umeona bagamoyo peke yao, au baadaya kumbwatukia waziri kwenye matokeo mabaya sasa unakuja nyumbani kwao ee.

Je unajua na uhakika na usemalo? Ukubwa wa Tanzania ni km za mraba 945,203 km² zaidi pata hapa

Districts of Tanzania - Wikipedia, the free encyclopedia je umeiona bagamoyo tu, kwa akili yako Bagamoyo ndio yenye matatizo haya pekee, au kwa kuwa waziri ni mbagamoyo? kaa mbali baba au pitia hapa

Au tafuta kazi ya kufanya

ova
 
We ushasema wanafunz hawana nidhamu kiasi kwamba wanawatishia walimu!sasa mwalimu akafanye nn shuleni?unataka wakauwawe?hata ningekuwa mimi nisingeenda kazini.then jua kuwa walimu wanafanya kazi kutokana na pesa wanayolipwa.so usiumize kichwa ndugu yangu
 
mwl muoneeni tu jibu lake mtalia, mnawanyanyasa hawa watu kwa nini? kil kitu mwl kila kitu yeye! why give them space
 
Back
Top Bottom