Nielimishe: Kwanini nilipe kodi kabla hata sijaanza biashara?

Napoleone

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2012
Posts
10,087
Reaction score
16,036
Wakuu,

Ni hayo tuu, nahitaji elimu hapa maana ninachojua mimi kidogo ni kodi ya mapato inakatwa kwenye faida sasa hata biashara sijaanza ndo nafanya paperworks ila nahitajika kulipa hilo kadirio.

Nimekua nalipa hivi kipindi cha nyuma ila leo imenibidi nijiulize hili swali, nadhani vyuma vimekaza sana.
 
Taxation system yenyewe kwa Tanzania hii hata haileweki.

Sera zenyewe za kodi zinabadirikana kulingana na size ya budget.

Sheria za kodi wanaozitunga ndio hao akina Ole sendeka na wengine ambao hawajawahi kufanya hata biashara.

Tax base yenyewe inayokusudiwa haijulikani kama ni makampuni au watumiaji wa mwisho wa bidhaa.

Utekelezaji wa ulipaji kodi wenyewe unaendeshwa kimabavu tu hakuna busara hata kidogo.

Ukiongelea suala la kodi Tanzania ni pasua kichwa na hakuna mtu anaeweza kukupa jibu/Maelezo ya kuridhisha na yenye mantiki.

Ngoja na mimi nisubiri majibu.
 
Hicho ni kishika uchumba cha ndoa kati ya mfanyabiashara na Zakayo!
 
Hicho ni kishika uchumba cha ndoa kati ya mfanyabiashara na Zakayo!
Lakin wale ma giant hua wana wa exempt 5yrs au sio.kwel hohehahe ataendelea kua hohehahe milele,..nahis Tz sio land of oportunities,..kwa hustle zangu hiz nadhan ningekua china au US ningekua na networth ya kama 250mil USD
 
!
!
"Kuna Muda Nawaangalia Ninyi Mnaotaka Kufanya Biashara Halafu Nasema Hiiiiiiiii"
Lakin wale ma giant hua wana wa exempt 5yrs au sio.kwel hohehahe ataendelea kua hohehahe milele,..nahis Tz sio land of oportunities,..kwa hustle zangu hiz nadhan ningekua china au US ningekua na networth ya kama 250mil USD
 
Lakin wale ma giant hua wana wa exempt 5yrs au sio.kwel hohehahe ataendelea kua hohehahe milele,..nahis Tz sio land of oportunities,..kwa hustle zangu hiz nadhan ningekua china au US ningekua na networth ya kama 250mil USD
 
Lakin wale ma giant hua wana wa exempt 5yrs au sio.kwel hohehahe ataendelea kua hohehahe milele,..nahis Tz sio land of oportunities,..kwa hustle zangu hiz nadhan ningekua china au US ningekua na networth ya kama 250mil USD
Mchumba mwenye hela nyingi anabembelezwa ili asikimbie!
 
Lakin wale ma giant hua wana wa exempt 5yrs au sio.kwel hohehahe ataendelea kua hohehahe milele,..nahis Tz sio land of oportunities,..kwa hustle zangu hiz nadhan ningekua china au US ningekua na networth ya kama 250mil USD
Tanzania haijawahi kuwa land of opportunities isipokuwa ni land of opportunists tu.

Tax holiday ni muhimu kwa mfanya biashara yeyote haijalishi ni mdogo au mkubwa, cha kushangaza hapa tanzania hiyo favor wanapewa wawekezaji wa kubwa tu tena wa kigeni(hahahha), wakati nyie wadogo mnalipa kodi tangu siku ya kwanza mnafungua biashara mpaka siku zinakufa.

Tanzania na afrika kwa ujumla kuna changamoto nyingi sana zisisokuwa na msingi kibiashara, mwana mama Forolusho Alakija ambae ni bilionea wa pili wa kike barani afrika, aliwahi kusema

"Mafanikio utakayopata ndani ya US, ukija afrika hili kupata mafanikio yale yele itakubidi uongeze juhudi mara saba ya zile ulizokuwa nazo US"

Akimaanisha kuwa afrika ni kugumu sana mara saba ya marekani. Kwa hiyo mkuu kama wewe kweli ni hustler basi nakuunga mkono pengine ingekuwa mbali sana kwa nchi zinazoeleweka.
 
The rule of thumb is "fanya biashara kwanza kodi utalipa baadae biashara ikikubali".
 
Mfumo wa kodi Tz ni kandamizi, hautoi fursa ya kuanzisha na kuendeleza biashara hasa kwa wenye mitaji midogo... Haiingii akilini kabisa Serikali inayotaka watu wajishughulishe ili kuinua maisha yao na kuchangia Pato la taifa wananyimwa nafasi ya kuanza vizuri... Haina haja ya kodi kwanza.. Kishika uchumba ilihali mtaji wenyewe ni ngumu kupata...ukitaka MKOPO bank wanataka biashara iliyokwisha anza... Sasa TRA mnatakeje kishika uchumba... Ni sawa lkn hio inawarudisha nyuma watu kuanza business... Nadhani serikali isajili kila biashara inayoanza.. Ifanye monitoring kwa mwaka mmoja, ndipo kodi ianze! Hakika wengi watafanya na hawatakwepa kulipa kodi.
Sasa kishika uchumba kinatangulia... Biashara inashindwa kabla mwaka haujaisha...mfanyabiashara anakuwa kapigwa
 
Short and clear..
uwezi ku register business na kulipia business license bila kuanza ku operate....[HASHTAG]#kwa[/HASHTAG] mtazamo wa tra utakua unaleta tax avoidance
pili huwezi kumake loss in 3 conserkative years, maana kama biashara ni hasara na unafanya lazma kuna unachonufaika,,so utalipia kodi pia ya mapato ..[HASHTAG]#kwa[/HASHTAG] mtazamo wa tra utakua unaleta tax avoidance
 
Ushawai fanya biashara?wew ni mfanya biashara?au unaongea na hujui hata unachoongea..kodi ya mapato maana yake nin? Tuanzie hapo kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…