Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Kumradhi sana Mangi hapa dukani najua wewe kazi yako ni kuuza Vocha sio kushauri, samahani Wateja wenzangu najua nyote mna haraka ila mniwie radhi kidogo maana nami ni Mteja na ni Mfalme au sio[emoji3]
Mangi nipate bando la mtandao gani hapo ili nipate network vizuri, maana mtandao wangu huu sioni zile status za Wadau wangu pale WhatsApp, sioni zile kashfa za kuwa Simba atapigwa tena tano tano, nambie Mtandao gani nikiweka nitaziona Status zao.
Mama hapo nyuma yangu usinune najua una haraka unataka upate sukari ukapike Vitumbua Mzee Mpili anasubiri, ila acha Mangi ananiambie bando la Mtandao gani nitaweza kupata kuzipokea tena zile Voicenote za kejeli na dhara, Voicenote za vicheko kutoka kwa wananzengo kuhusu Simba.
Mangi naomba nitajie haraka maana kuna Kaka pembeni yangu kanuna, nahisi anataka Mpira wa kiutu uzima ana kipengele magetoni[emoji3], ila we nitajie tu Bando la Mtandao gani linafaa ili nione post za Mabraza huko Instagram, posts za kashfa na dharau nyingi maana sasa sizioni.
Kiukweli nimerefresh sana simu, nahisi ni mtandao tu! Mangi nina shida sana na bando, nione clip za Clatous Chama, nasikia goli la nne alitisha kama anapiga na beki wa Vita alidondoka kama embe bolibo kutoka mtini, Mangi nipe Vocha niwaone Vita walivyochoka kama wanapanda vilima vya Msanga.
Bando zuri kutoka Mtandao mzuri Mangi kunradhi nishauri, au kama namchelewesha sana Dada pembeni anataka taulo la kike maana Simba wameanza kucheza huenda, ila nikipata bando nataka kumwona Sergie Pascal Wawa, nasikia pasi ya jana ya Kroos hata yeye anazipiga sana.
Kama nawakera Wateja wenzangu basi mniwie ni basi tu naona fujo zimepungua, sioni Status za madongo WhatsApp, sioni post za majungu Instagram na sioni caption za kifedhuli pale Twitter[emoji3], huenda ni Network ya huu mtandao, MANGI NIPE VOCHA nithibitishe.
MANGI NASEMA NIPE VOCHA[emoji3]