Niendelee kumfatilia?

Niendelee kumfatilia?

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
4,854
Reaction score
1,129
Habari zenu Jf, Naomba ushauri wenu,, ni hivi kuna msichana ambaye nimempenda na nimeshaanza kutengeneza ukaribu naye. Habari niliyoipata jioni ya leo ni kwamba rafiki yangu wa karibu amewahi mpenda sana huyu binti, lakini hakufanikiwa kumpata baada ya kumfatilia kwa muda mrefu. Kwa kifupi bado sijamweleza lengo langu. Hofu niliyonayo, ikitokea nikampata na kuwa naye, huyu rafiki yangu atanichukulieje na atajisikiaje?{hajawah kuniambia hili suala}.
 
we hujampenda huyo..
ukimpenda mtu hata uambiwe mumewe kafa na ukimwi
na bado utamfatilia...
au hata ukiambiwa baba yako amepita na bado utamfata...
 
inawezekana eti? Nimekusoma
 
Changamka mkuu mueleze hisia zako ulizonazo kwakwe na khs huyo jamaa yako kama hajawai kukueleza hisia alizonazo kwake haina shida nafikiri atachukulia poa make kama kweli alikuwa anampenda angemwambia hata kabla hujawa na hisia yeyote kwa huyo dada
 
aisha na mimi
ntakuja kukueleza ya kwangu pia...lol
 
Usiishi kwa kuhofia watu!
Kama una nia njema kwake fatilia.
 
Habari zenu Jf, Naomba ushauri wenu,, ni hivi kuna msichana ambaye nimempenda na nimeshaanza kutengeneza ukaribu naye. Habari niliyoipata jioni ya leo ni kwamba rafiki yangu wa karibu amewahi mpenda sana huyu binti, lakini hakufanikiwa kumpata baada ya kumfatilia kwa muda mrefu. Kwa kifupi bado sijamweleza lengo langu. Hofu niliyonayo, ikitokea nikampata na kuwa naye, huyu rafiki yangu atanichukulieje na atajisikiaje?{hajawah kuniambia hili suala}.

...kama imeandikwa uwe naye itakuwa tu, rafiki yako atakuwa shemeji yake.
Jali hisia zako kwanza.
 
we hujampenda huyo..
ukimpenda mtu hata uambiwe mumewe kafa na ukimwi
na bado utamfatilia...
au hata ukiambiwa baba yako amepita na bado utamfata...
mmmh,the boss,the boss,the boss.una majibu ya kufyatua kweli kweli.ingawa yana ukweli
 
rafiki yako akishindwa ndio sababu nzuri
ya wewe kuingia...
je angefanikiwa?ungeingia????????

unatakiwa ushukuru kuwa kashindwa
sasa ingia wewe
mkishindwa wote aibu

Ndo maana nakukubali,huu ndo ukweli,sioni sababu ya kuhofia,kama kweli umempenda,nenda kamu-approach....mtazungumza,atakujibu yataisha,pengine nawe pia utakataliwa wala huyo rafiki yako asijue.....so jiamini,songa mbele!!
 
...kama imeandikwa uwe naye itakuwa tu, rafiki yako atakuwa shemeji yake.
Jali hisia zako kwanza.
Kabisa mtu unaangalia hisia zako, unajua mambo yote ni mipango ya Mungu, na kila kitu kinatokea kwa makusudi, yaani mtu unaweza tu kuwa daraja la watu wengine waliopangiwa kuwa ppamoja kukutana, ndio maana utaona rafiki yako mkubwa wakati mwingine ndio anaishia kuwa mume/mke wa mchumba ako uliyetegemea kufunga nae ndoa, na wakaishi maisha mazuri tu na wao ndio wakaja kuwa perfect match
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Ndo maana nakukubali,huu ndo ukweli,sioni sababu ya kuhofia,kama kweli umempenda,nenda kamu-approach....mtazungumza,atakujibu yataisha,pengine nawe pia utakataliwa wala huyo rafiki yako asijue.....so jiamini,songa mbele!!

na inawezekana rafiki alikataliwa
ili yeye apewe nafasi
 
Nakushauri achana nae huyo demu.Ukibisha yatakayokupata,usije kunilaumu baadaye
 
Acha uoga wa kukataliwa kijana ndo uanaume huo. Hapo huogopi rafiki yako wala nini, unaogopa fupa lililomshinda rafiki yako.
 
kumwagwa siyo ishu na sijawah ogopa hata siku moja.
 
Wewe mfuatilie tu achana na habari za huyo rafiki yako!
 
Back
Top Bottom