Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
@Nifah Swaiba, Rafiki. Kuna watu kwetu ni ngumu kukubaliana na hili mliloliamua. Twatamani tuwaitishe pamoja ili tu solve hili jambo. Kwakuwa mmeamua kwa kuridhia wenyewe pasi sisi kuwashauri basi ikawe Njema kwenu.


Ila Isigeuke vita baina yenu.
 
Wewe ni extrovert yeye no introvert mkashindwana kiasili!

Huyu ni mkimya anawaza aandike kuhusu Somo jasusi fulani,lakini wewe Trend reader sanguine mcheshi ukajikuta unapiga story mwenyewe halafu ukataka umbadili awe mcheshi mwenye kuelewa mwitikio wa hisia zako na unapotaka uguswe Kihisia ukakuta ndio kwanza "ujasusi sebuleni" akiandika!

Aiseh,

Poleni sana!
Ndo ninachopitia mie hapa, baba tamu ang ni introvert, yaan anawaza mambo makubwa makubwa nae km jasusi hivii,

Kila nikitaka kumbadilisha, anaishia kuniambia mie ndo nibadilike niendane na yeye,hata sielewiii.
Nachokaaa wallah, ila simuachiii kwakee nimefika na mabegi nishatua.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mnapendana? Nae akae 4 years bila ndoa akuachie tu zawadi ya kua single maza

Uwe single maza kwa wanaume wawili?
Labda kama wewe ndo una matatizo wanashindwa kukuoa

lkn kama upo sawa, 2024 usiishe bila ndoa cz mnazeeka 30's hamna utoto wakuganda kwenye uchumba

Wewe ni mzuri sanaaaa, nilivyokuona hadi mimi nilichanganyikiwa sembuse mwanaume.

NB: Sijawahi kuolewa, Sio mshauri wa Ndoa.
Nifah
Kwa huyu kila kitu kitaenda sawa, tuna mipango mingi na zaidi tunapendana sana.

Muhimu ujue sio mpya, tunajuana vyema.

Asante mwaya
 
Ndo ninachopitia mie hapa, baba tamu ang ni introvert, yaan anawaza mambo makubwa makubwa nae km jasusi hivii,

Kila nikitaka kumbadilisha, anaishia kuniambia mie ndo nibadilike niendane na yeye,hata sielewiii.
Nachokaaa wallah, ila simuachiii kwakee nimefika na mabegi nishatua.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yeye ana waza ki Nietzsche, wee una waza ki lokole😀😂
 
Back
Top Bottom