hayo machemical usikute ndio yanayozidisha, Halaf pia hujaeleweka ngozi yako ni ya mafuta au kavu, kwanza umesema ngozi kavu...halafu chini umesema imejaa mafuta, si kila unachoambiwa ndo ufanywe hasa hizo tube, labda vitu vya asili vinakuwa vingi havina madhara, kwa kifupi, mie nitakupa dawa za asili ambazo husaidia ngozi kuwa nyororo kwanza changanya Manjano na liwa (Msio) paka uson jisugue kama unatoa nongo na baadae paka halafu kaa nayo hata nusus saa hata lisaa kulingana na wewe unavyotaka au nafasi yako, halafu nawa uso wako paka mafuta unayotumia, ila kwa sasa paka lotion za kawaida ambazo sio kali.
Na pia unaweza changanya Asali, Mtindi na maji ya limao, jipake usoni kamaa muda wa dakika 15 halafu osha uso wako, au pia unaweza tumia mtindi na manjano pekee.
Jitahidi pia kunywa maji mengi, epuka kulala na mamake-up, na vipodozi vyenye machemical kwa sasa pumzisha fanya vitu vya asili. habba soda nayo ni nzuri kusugulia uso inakuwa kama ndo scrub yako, ila hakikisha ukisugua na habba soda, inabidi manjano na msio usijisugue paka tu na ikikauka osha. Na hata mapumba ya mahindi yale ukiyaroweka na maji halafu jipake usoni mpaka shingoni, yaache kidogo yakauke ila si sana halafu anza kujisugua ukimaliza kaoge, week tu au week 2 utaniambia jinsi sura itakavyokuwa nyororo.
Nadhani ukimaliza kupaka hivi vitu vya asili unaweza pia kutumia lotion au cream yoyote ya cocoa butter.
Wanawake wengi waki-comoro wanakuwa na ngozi lainiii nakupendeza sabab ya hii liwa kwao ni kama asili kwao.