Nifanyaje ili mchuzi uwe mzito

Tungule si ndo nyanya chungu or? na je ukisagia kwenye mchuzi nilikuwa nauliza si utakuwa mchungu balaa?

Hahhahahah doh tunaongea lugha tofauti.
Tungule huko munaita nyanya
Nyanya chungu huku tunaziita hivyohivyo nyanya chungu nikisema tungule nimekusudia nyanya au tomato!
 
Hahhahahah doh tunaongea lugha tofauti.
Tungule huko munaita nyanya
Nyanya chungu huku tunaziita hivyohivyo nyanya chungu nikisema tungule nimekusudia nyanya au tomato!

hahahah yaani ulikuwa umeniacha hoi

mie nikajua llloh sasa nyanya chungu tena zisagiwe kwenye blender hatari

Kwa hiyo Tungule ni Kiswahili? duh
 
Qqxqdq,iwp:mfpdfiiwiwplipiipwilwpwliwiwiiwwwiiiiiwwwwwllwlwllllllllllllllliiilllllwii
 
First Lady 1 "Tungule" kwa kiswahili cha pwani tunamaanisha nyanya(tomatoes) zile za uchingu tunaita "ngogo"

tungule...lol! hicho kiswahili sijawahi kukiskia, itakuwa lugha flani nyingine. ngongo ndiyo nyanya chungu?
 
tungule...lol! hicho kiswahili sijawahi kukiskia, itakuwa lugha flani nyingine. ngongo ndiyo nyanya chungu?

Ndio mkuu! kumbuka kiswahili ni bahari pana kuna lafudhi na lahaja lukuki!
 
usisahau unga wa ngano kidogo, nilishawahi kufanya kazi kwenye hoteli moja kubwa, yaani kila mchuzi uliongezwa unga wa ngano na ulitoka fresh
 
Tunguli = Tungule
Ndo nyanya in Zanzibar
Ukienda Zanzibar ndo lugha yao mara ya kwanza kuwa huko 19... Nilikuwa najichanganya kweli

loh, ama kweli lugha pana, hata mimi nikitumwa tungule nitanunua nyanya chungu au kitu chochote cha kufanana nahicho lakini si nyanya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…