Nifanyaje ili Niwe na Uwezo 'Power' ?

Ndikwega

R I P
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,979
Reaction score
5,527
Salaam Wakuu!

Naleta kwenu hii hoja, yamkini wapo wengi wanajiuliza swali kama hili. Kiukweli sina jibu, ila nimeleta huku kuna watu watasaidia kulifumbua hili.

Jambo la kujiuliza je Kuna watu waliumbwa Wanyonge na wengine kuwa na Nguvu ama Hodari, yaani ambao hawaguswi hovyo? Aidha kuwa na Nguvu za Utiisho ama za kuamuru jambo fulani kwako lisiwe tatizo kulifikia!

Kuna Nguvu za Mtu kuamuru jambo fulani lisitendeke hata kiimani likiwemo, mfano katka nguvu za Giza, ama kuwa na Ushawishi wa Kihoja mpaka unasikilizwa na kutekelezwa wazo lako.

Katika mfumo wa Dunia naamini kuna Mambo mengi saana ambayo wanadamu tunaweza kuyafanya hata kushangaza wengine. Sasa hoja yangu nifanyaje ili kupata huo Uwezo?

How can I become a Superiorman?

Ahsanteni,na Karibuni!
 
Taka sana utakuwa nazo
Ongeza shauku yako

Ukiumiza kichwa sana kuzitaka lazima uzipate.
 
Source of power

Money..... Tafuta hela mkuu utaamisha mlima

Political authority...... Ingia CCM, jipendekeze, utamfikia au hata kumpita bashite

Make yourself scarce/Posses something scarce..... Uchache siku zote unaongeza thamani ya mtu hatimaye unaongeza nguvu yake
 
[emoji115] [emoji115] [emoji115] [emoji115]

Nakubaliana na wewe maana miaka kadhaa iliopita niligombana na rafiki yangu na tulikuwa tunasaidiana sana baada ya kutofautiana aliapa hatokaa snipe chochote na wala ukaribu nae upotee

Niliingia nyumbani siku kadhaa nili Fanya meditation ya kutatua lile jambo kwa kina nilitumia kama DKK 45 hivi nilibishana nae sana kwa mawazo ya kihisia
Mwisho nikifanikiwa kuyajenga nilimaliza meditation yangu kesho yake from some where alinitafuta na kuniambia nije tuonane rafiki na nichukuchue mzigo Fulani niliokuwa nimemwomba nilimwendea na kuongea nae kama vile hatukuwai kugombana magombano Yale hii power inanguvu za ajabu sana
 
Nifundishe hiyo meditation nina mambo mengi ya kutatua
 
Mungu ndiyo kilakitu kijana, mtegemee yeye and you'll become a Super human,
 
Pesa tu ndugu, unakuta kwenye familiya MTU mmoja ana pesa yaan hata afanye ujinga hakuna wakumsema wanamuona ndio mungu wao.
 
Nguvu unazo ila hujiamini. Tulia. Omba kwa dini yako.
 
Tafuta humu mbona kuna nyuzi nyingi zinaelezea jinsi ya kufanya meditation au mwambie mshana akuelekeze but yahitaji moyo sana kuijua coz sio kitu simple ila kina faida sana
Ni kweli yaitaji nguvu na moyo
 
Msanii Nas katika wimbo wake maarufu I can,
Alisema "You can be anything in the world... but nothing comes easy it takes much practice"

Jambo la kwanza na la muhimu ni kutambua udhaifu wako katika
maeneo mbali mbali kisha unayafanyia kazi kisawa-sawa.

Jambo lingine ni udadisi na shauku,ili kutambua Mambo mengi na kuwa na maarifa kichwani udadisi ni kitu kikubwa,udadisi wa maswali mbali mbali yawe ya kimaisha au zaiidi,unayatafakari unafikirisha ubongo, kisha unayafanyia kazi kisawa kisawa pia Usomaji vitabu tofauti tofauti vinavyuhusu Maisha,Biashara,Elimu,Sayansi n.k Mfano ushawishi wa hoja huwezi kuwa mjenga hoja mzuri na mwenye ushawishi kama unavitu vichache kichwani na njia ipi unayotumia kufikisha kufikisha hoja zako.

Pia uchaguzi sahihi wa eneo unalotaka kulifanyia kazi kisha inalitengea muda wa kutosha. Mfano magician maarufu bwana Steven "Dynamo the magician" yeye aliaanza kufatilia na kutenga muda wake tangu akiwa na umri mdogo alijifunza na kufanya mazoezi katika masuala ya magic hivi sasa anatambuliwa na wengi kama the best magician,hivyo kila jambo linahitaji muda,bidii,nidhamu na kufanya mazoezi sana.


Shukran!!Yangu ni hayo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…