Kafanye yafutatayo halafu bada ya mwezi mmoja leta mrejesho hapa...
-Tumia asali kuunga kwenye chai badala ya sukari na tumia brown bread badala ya white bread kwa ujumla wakati wa chai au kifungua kinywa pamoja na soya badala ya majani ya chai, Hii husaidia ku-utrick mwili kwani hukuwezesha kujisikia umeshiba wakati woote na kupunguza tabia ya kula kula na kuufanya mwili uanze kuyeyusha mafuta ya mwilini ya ziada kwa ajili ya kujipatia nguvu/energy
-Fanya mazoezi ya kata tumbo au mazoezi yoyote ya kujenga misuli kwani husaidia mwili kuyeyusha mafuta kwa ajili ya energy ya kuijenga hiyo misuli
-Chukua simu yako(kama ni mchina) kwa sauti yako mwenyewe rekodi maneno yanayohamasisha mwili kupunguza kitambi na urekodi simple statements katika present tense kwa lugha yoyote,
Mfano : Kitambi kinapungua siku kwa siku, kiwango cha mafuta yangu kinapungua kila kukicha, Mimi ni mtu mwenye afya njema na nisiye na kitambi, Kitambi ni kitu cha hovyo katika maisha nk.
Sikiliza muda wowote angalau mara mbili kwa siku na si lazima uweke sauti ya juu sana, hata kama inanong'ona ubongo unaweza kusikia na kutambua sauti yako hata kama wewe huisikii. Hii inasaidia kuufanya ubongo wako uamini kuwa unapewa command ya kushughulika na mafuta mwilini, BELIEVE ME baada ya wiki nne utashangaa matokeo yake(technique hii wanaitumia wanamichezo wa kimataifa hasa timu za mpira za uingereza na wanariadha)
-Angalau mara moa kwa wiki pata funga yako moja ya juisi natural hasa apples na avocardo yanayosaidia kuondoa sumu mwilini hasa zile zinazojificha kwenye mafuta kama lead na vyuma vingine vizito(heavy metals)..
-Hakikisha wakati wa kula unatafuna chakula kwa muda mrefu kabla ya kukimeza, usile kama mbwa fasta fasta, Chakula kikitafunwa vizuri humengenywa vizuri na kuutosheleza mwili na hupunguza haja ya kula sana kitu kinachoupa mwili muda na nafasi ya kujisafisha wenyewe. Tafiti za hivi karibuni zinaonesha 60% ya chakula anachokula mtu hutoka mwilini bila kumeng'enywa na hii husababishwa na kutokutafuna chakula vizuri na kwa muda mrefu kwani mmeng'enyo wa chakula mara zote huanzia kinywani
Mnegine ni ya kawaida kama kuepuka kula vyakula vya mafuta kupita kiasi, vyakula vya makopo na vyenye sukari nyingi na yoote wanayoshauri wataalamu wa afya....
Usiniulize taalauma yangu we kafanye baada ya mwezi njoo utoe ushuhuda hapa....