Nifanyaje nipende tena

Nifanyaje nipende tena

Kuna binti nilimpenda mno wakati nipo shuleni. Mimi nikiwa form six yeye yupo form two. Kipindi hicho sikuwahi mwambia hisia zangu kwani nilimuona kama mtoto bado, nikahisi ningemvuruga kiakili kumuambia mambo ya mapenzi. Pia nilihofia ningejivunjia heshima niliyojitengeneza shuleni hapo kwa kumtongoza mtoto hali mimi Kiongozi wa dini

Nikahitimu form six na kujiunga na chuo yeye nikimwacha shuleni. Tukapoteza mda mrefu sana.

Baada ya kitambo hicho siku nikapata mawasiliano yake kupitia kwa jamaa yangu. Nikamtafuta. Tukaanza kuwasiliana mara kwa mara. Kutakiana siku njema, usiku mwema, karibu chakula nk. Chombeza Chombeza hizi ndio hisia zile za zamani zikafufuka tena. Sikutaka kupoteza muda nikamuelezea hisia zangu juu yake ambapo alikubali tuwe na uhusiano.

Nilikuwa yule yule. Nilimpenda mno. Mno yani. Hata nashindwa kuelezea. Hakuhitaji kitu nikashindwa mpatia. Upendo nilioanza nikiwa mtu mzima ninayejitambua.

Upande wake bint ilinidhihirikia wazi kuwa hakunipenda kihivyo, ila nilijipa moyo kuwa huenda upendo utaongezeka kadri siku zitavyokwenda.

Kipindi hicho jamaa zangu wengi walikuwa wanaoa. Binti huyu nami nikaona ananifaa kabisa. Basi baada ya uhusiano wa muda mfupi nikamshawishi nipeleke posa kwao, ambapo alikubali. Nikaongea na wazee wangu, posa kweli ikapelekwa.

Sasa siku wazee wanaenda kufata majibu ya posa, nikiwa natumaini makubwa ghafla jioni moja binti akanitumia sms ndefu akiniarifu kuwa anaomba uhusiano wetu uishe kwani tayari ana mtu mwingine moyoni mwake kabla yangu na hawezi kumuacha. Akaniomba radhi kwa kutonijuza mapema. Lawama za hapa na pale bado alisimamia pale pale

Mda huo nilikuwa nimeshawatangazia jamaa zangu kuwa waandae michango nipo kwenye hatua za mwisho za kujitwalia jiko. Bimkubwa pia alikuwa ashaanza kuwaambia marafiki zake juu ya hili.

Upande wa wazazi wa binti walikuwa wamekubali na kuridhia kabisa, binti ndio alikuja kukengeuka

Sikuwa namna bali kukubali hali halisia. Sikutaka kulazimisha penzi.upande wa wazee nikatufuta sababu za uongo nikwaambia, mwisho nikaahirisha ile posa. Wazee wakakubali

Moyo wangu uliumia baada ya hili tukio. Nilijikuta nimeanza kutumia madawa ya kulevya kwa maana hata usingizi nilikuwa nakosa. maumivu moyo yalikuwa makali mno kwangu. Huu ulikuwa uhusiano wangu wakwanza nikiwa najitambua

Baada ya muda mrefu kupita niliweza kurudi katika hali yangu ya kawaida na madawa nakaacha

Sasa shida ni kuwa ni mwaka wa nne sasa nashindwa kupenda tena. naona ni hali ya Kawaida tu kuwa single. Wadogo zangu wanaoa kila siku ila mim sina habari na wala hainitatizi. Sina hamu kabisa na uhusiano. Nifanyaje nipende tena maana siku kusogea.
Mimi nadhani huyo demu alikua mjanja zaidi yako na alikua ameshafunguka kiakili kuliko wewe, japokua wewe ni mkubwa kuliko yeye.

Wakati ulipomtafuta na kuanzisha nae mahusiano, yeye alijua unataka kumega kisela uende zako kama watu wengine. Ndio maana akakukubalia na wala hakukuambia kama ana mtu. Cha ajabu wewe badala ya kupiga utembee zako mbele, ukaanza mambo ya kushangaza ya kuanza kutangaza ndoa na mtu ambae kiuhalisia ulikua humjui, hujui maisha anayoishi, huna taarifa zake etc. Wewe ulidhani kwamba jinsi ulivyomuacha form 2 utamkuta yuko palepale anakusubiri, kumbe mwenzio anaendelea na maisha yake wewe ndio uko stuck in the past.

Nadhani alifanya la maana kukupiga chini unaonekana ungekuja kumsumbua tu na mapenzi yako ya kitoto.
 
Pole sana mkuu, nadhani alichokosea huyo binti ni kutokukwambia mapema, japo uamuzi wa kukwambia ni mzuri sana na nadhani kama ungeingia kwenye ndoa nae, yangekukuta zaidi ya hayo.

Kuhusu kupenda tena, huo ni uamuzi wako. Inabidi ukubaliane na hali kwamba yule ameshaondoka, na past yako haiwezi kuharibu future. Najua wapo girls wengi karibu yako, jaribu kuufungua moyo wako. Ruhusu mtu aingie, hata kwa urafiki tu. Moyo una kawaida ya kupambania kitu unachotaka, so ukiwa na mtu karibu ni rahisi moyo kufunguka.

Nje ya mada, huyo binti aliyekutosa muda wa kupeleka posa, Yuko wapi now?
Shukran mno mkuu
 
Mimi nadhani huyo demu alikua mjanja zaidi yako na alikua ameshafunguka kiakili kuliko wewe, japokua wewe ni mkubwa kuliko yeye.

Wakati ulipomtafuta na kuanzisha nae mahusiano, yeye alijua unataka kumega kisela uende zako kama watu wengine. Ndio maana akakukubalia na wala hakukuambia kama ana mtu. Cha ajabu wewe badala ya kupiga utembee zako mbele, ukaanza mambo ya kushangaza ya kuanza kutangaza ndoa na mtu ambae kiuhalisia ulikua humjui, hujui maisha anayoishi, huna taarifa zake etc. Wewe ulidhani kwamba jinsi ulivyomuacha form 2 utamkuta yuko palepale anakusubiri, kumbe mwenzio anaendelea na maisha yake wewe ndio uko stuck in the past.

Nadhani alifanya la maana kukupiga chini unaonekana ungekuja kumsumbua tu na mapenzi yako ya kitoto.
Dahhhh
 
We jamaa hujitambui. Yani jambo ambalo lilikuingiza kwenye matatizo wewe bado tu unataka kuelekezwa jinsi ya kurudia kulifanya?


Achana na mambo ya mapenzi. Tafuta shughuli nyingine ufanye.
Ila we jamaaa big brain sana
Sina Hizo dhamira anazofikiria mkuu. Wengi tuna matatizo ya kisaikolojia tunayaleta humu walau tusaidiwe hata kwa mawazo.
 
Hongera sana mkuu huo ndo umwamba sasa mambo ya hisia za kupenda achia wamama. KATAA NDOA NI UTAPELI
 
Ikifika wakati wako sahihi wala hilo swala halitokuwa yaani ndio hivo tuu moja kwa moja
 
Back
Top Bottom