Omerta
JF-Expert Member
- Jan 3, 2016
- 5,957
- 7,505
Nasema mshukuru sana huyo Binti, narudia tena mshukuru sana huyo Binti- angekuja kukutesa sana kwenye ndoa , yaani angetumia hizo hisia zake kukunyuka sana- believe me son , just find a decent gal mjenge familia achana na mambo ya kupenda wanawake. It is too late for some of us but ,it is never late for you.Kuna binti nilimpenda mno wakati nipo shuleni. Mimi nikiwa form six yeye yupo form two. Kipindi hicho sikuwahi mwambia hisia zangu kwani nilimuona kama mtoto bado, nikahisi ningemvuruga kiakili kumuambia mambo ya mapenzi. Pia nilihofia ningejivunjia heshima niliyojitengeneza shuleni hapo kwa kumtongoza mtoto hali mimi Kiongozi wa dini
Nikahitimu form six na kujiunga na chuo yeye nikimwacha shuleni. Tukapoteza mda mrefu sana.
Baada ya kitambo hicho siku nikapata mawasiliano yake kupitia kwa jamaa yangu. Nikamtafuta. Tukaanza kuwasiliana mara kwa mara. Kutakiana siku njema, usiku mwema, karibu chakula nk. Chombeza Chombeza hizi ndio hisia zile za zamani zikafufuka tena. Sikutaka kupoteza muda nikamuelezea hisia zangu juu yake ambapo alikubali tuwe na uhusiano.
Nilikuwa yule yule. Nilimpenda mno. Mno yani. Hata nashindwa kuelezea. Hakuhitaji kitu nikashindwa mpatia. Upendo nilioanza nikiwa mtu mzima ninayejitambua.
Upande wake bint ilinidhihirikia wazi kuwa hakunipenda kihivyo, ila nilijipa moyo kuwa huenda upendo utaongezeka kadri siku zitavyokwenda.
Kipindi hicho jamaa zangu wengi walikuwa wanaoa. Binti huyu nami nikaona ananifaa kabisa. Basi baada ya uhusiano wa muda mfupi nikamshawishi nipeleke posa kwao, ambapo alikubali. Nikaongea na wazee wangu, posa kweli ikapelekwa.
Sasa siku wazee wanaenda kufata majibu ya posa, nikiwa natumaini makubwa ghafla jioni moja binti akanitumia sms ndefu akiniarifu kuwa anaomba uhusiano wetu uishe kwani tayari ana mtu mwingine moyoni mwake kabla yangu na hawezi kumuacha. Akaniomba radhi kwa kutonijuza mapema. Lawama za hapa na pale bado alisimamia pale pale
Mda huo nilikuwa nimeshawatangazia jamaa zangu kuwa waandae michango nipo kwenye hatua za mwisho za kujitwalia jiko. Bimkubwa pia alikuwa ashaanza kuwaambia marafiki zake juu ya hili.
Upande wa wazazi wa binti walikuwa wamekubali na kuridhia kabisa, binti ndio alikuja kukengeuka
Sikuwa namna bali kukubali hali halisia. Sikutaka kulazimisha penzi.upande wa wazee nikatufuta sababu za uongo nikwaambia, mwisho nikaahirisha ile posa. Wazee wakakubali
Moyo wangu uliumia baada ya hili tukio. Nilijikuta nimeanza kutumia madawa ya kulevya kwa maana hata usingizi nilikuwa nakosa. maumivu moyo yalikuwa makali mno kwangu. Huu ulikuwa uhusiano wangu wakwanza nikiwa najitambua
Baada ya muda mrefu kupita niliweza kurudi katika hali yangu ya kawaida na madawa nakaacha
Sasa shida ni kuwa ni mwaka wa nne sasa nashindwa kupenda tena. naona ni hali ya Kawaida tu kuwa single. Wadogo zangu wanaoa kila siku ila mim sina habari na wala hainitatizi. Sina hamu kabisa na uhusiano. Nifanyaje nipende tena maana siku kusogea.
You are lucky dumb as* , Mwenyezi Mungu anakupenda sana.