Nifanye lipi kati ya haya mawilii? Nna milion moja na laki tano

dtv

Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
13
Reaction score
2
Hi wanajf naomba ushauri wa kifikra katika kujiendeleza kiuchumi kwan nina 1,500,000 na nina mpango wa either kununua boda boda niifanyie kazi mwenyewe au ninunue lain ya mpesa na tigo pesa nitoe huduma hiyo. nimegraduate ila ajira ni n shida. Mawazo yenu yatansaidia
 
Upo mkoa gan kwanza maana ushauri unaendana na mazingira...nsijekukushauri ununue ngalawa hafu ukute upo Dodoma..
 
mwenzenu anaombaushaur nyie mnamwambia aende kimboka.aghrrr.anza na boda,then wekamalengo ya m/tigo pesa.nadhani iz cool
 
Fanya biashara ya mazao mkuu.
 
Nenda kwa tb joshua...utakua poa
 
weka ofisi ya m/tigo pesa mkuu..bodaboda watakuua kama sio wezi basi huko barabarani. tafuta sehemu nzuri yenye watu na mzunguko wa pesa.
 
Mpaka tunaingia mitamboni hakuna aliyetoa ushauri wa maana, nikiripoti kutoka jf mimi ni jooooooooohhhhhhnnnnn malaaaaaatuuuu wa aiiitttvvvvvv.
 

mkuu bora mpesa au tigo pesa! bodaboda zenyewe zimeshaanza kuandamwa na serikali hasa jijini dsm, wameanza na kuzipiga marufuku kuingia katikati ya jiji! bora mpesa, tigo pesa hata airtel money hazina usumbufu!
 
mkuu bora mpesa au tigo pesa! bodaboda zenyewe zimeshaanza kuandamwa na serikali hasa jijini dsm, wameanza na kuzipiga marufuku kuingia katikati ya jiji! bora mpesa, tigo pesa hata airtel money hazina usumbufu!

kaka baada ya kumaliza chuo nikatafuta job ndani ya mwaka mmoja hola! nikanunua bdbd huwezi amini napaki mnazi mmoja ukweli huu ni mwaka wangu wa pili pikpik imenipa shamba, nyumba ya vyumba viwili, mke ajali zipo, wezi wapo na huo usemi tutafukuzwa tusifike mjini naona ni ndoto za mchana!!!!
 
Mkuu mi nakushauri bora ukomae na bodaboda tu coz kwa mpesa na tigo pesa mtaji Wako huo mdogo sana nasema ivo coz Nina experience na hyo biashara hlf dzain km oshafka mwisho coz commission zinapungua daily
 
Nenda kwa tb joshua...utakua poa

kwa tb joshua mbali, hapa hapa bongo kuna mzee wa upako; ana uwezo wa kuhamisha elnino iliyokuwa ipige tanzania na kuipeleka asia, anaweza kumuombea akapata chochote akitakacho.....

kushauri katika mada iliyoweka nadhani bodaboda ni mwanzo mzuri kwasababu atakuwa anapata pesa ya kila siku, baada ya hapo aweke pesa impe mtaji wa kubadili biashara.
 
Kwakuwa umeomba ushauri baina ya hizo biashara mbili nakushauri kama ifuatavyo.
TIGO PESA NA MPESA.
1. Unahitaji rent na ukarabati mahalia pa kufanyia biashara hiyo ambazo ni gharama na mtaji wako ni mdogo sana.
2. Cammision ni ndogo sana ukilinganisha na rundo la hela unalofanyia kazi mfano kupata faida ya commision,ya 20,000 inahitaji upate watu 100 waweke au kutoa hela kiasi cha wastan 25,000 ambapo mzunguko ni 2,500,000.
3. Risk ya kivamiwa
BODA BODA.
1. Boda boda ukipata dereva mzuri na ambaye ataweza kukuletea kiasi kisichopungua 8000 kwa siku 6 umapata 42,000 kila wiki. Siku moja ni ya service na kumwaga oil ili isichoke mapema
2. Itakuchukuwa miezi 7 Hela itakua imerudi na bado unaweza kuiuza si chini ya 1,000,000.
3. Haina kodi ya mwezi hakuna usumbufu
So nakushauri boda boda binafsi nilikuwa na boda boda mbili baada ya mwaka niliziuza nikaanza mpesa,tigo pesa hakunilipa sana nimeweka na stationery na studio ya passport size.
 

Tatizo haujasema uko wapi, mimi huwa napenda sana kuongea na watu ninapokuwa sehem, kuna jamaa kama wawili wanapaki ubungo niliwahi kuwauliza wanalaza kiasi gani, mmoja pikipiki ni yake alisema siku mbaya anaweza kubaki na 25K akishatoa gharama za mafuta, lakini siku ikiwa nzuri analala mpaka na 70 au zaidi. ukijua vijiwe vizuri unakuwa unakula buku tanotano hizo mpaka unachanganyikiwa, ONDOA UBISHOO!!! Pia kuna jamaa wa njombe alinishangaza anasema analala na 80-120K...hiyo skuamini mpaka nipate chanzo kingine. Pikipiki kuwa makini tu barabarani, uwe mstaarabu utakusanya pesa, baada ya mwaka kama utakuwa strict na unasave kwa hasira lazima utakuwa na kiasi kizuri cha kuanzia biashara nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…