Kwakuwa umeomba ushauri baina ya hizo biashara mbili nakushauri kama ifuatavyo.
TIGO PESA NA MPESA.
1. Unahitaji rent na ukarabati mahalia pa kufanyia biashara hiyo ambazo ni gharama na mtaji wako ni mdogo sana.
2. Cammision ni ndogo sana ukilinganisha na rundo la hela unalofanyia kazi mfano kupata faida ya commision,ya 20,000 inahitaji upate watu 100 waweke au kutoa hela kiasi cha wastan 25,000 ambapo mzunguko ni 2,500,000.
3. Risk ya kivamiwa
BODA BODA.
1. Boda boda ukipata dereva mzuri na ambaye ataweza kukuletea kiasi kisichopungua 8000 kwa siku 6 umapata 42,000 kila wiki. Siku moja ni ya service na kumwaga oil ili isichoke mapema
2. Itakuchukuwa miezi 7 Hela itakua imerudi na bado unaweza kuiuza si chini ya 1,000,000.
3. Haina kodi ya mwezi hakuna usumbufu
So nakushauri boda boda binafsi nilikuwa na boda boda mbili baada ya mwaka niliziuza nikaanza mpesa,tigo pesa hakunilipa sana nimeweka na stationery na studio ya passport size.