Habari zenu waungwana.Nina swala kichwani mwangu linanitatiza sana.Nawaza nichukue hatua gani lakini najikuta nakosa chakufanya.
Ni hivi,mwaka 2011 March nilianza mahusiano na binti mmoja ambaye alinitaka mwenyewe.At first moyo wangu ulikua mzito kukubali but kadiri mda ulivyo sogea alianza kuniingia moyoni taratibu.kipindi hicho nilikua advance na Huyo binti alikua na kichanga cha mwaka mmoja.
So mi niliendelea kukomaa na elimu{form5} binti akawa yupo home analea mwanae.Lakini nilivyo kua shule huyu binti alitoka kimapenzi na best friend wangu.Kama haitoshi mshikaji akaja kuniambia "demu wako Malaya achana nae Mimi nimesha mgonga" niliumia moyoni but nilijikaza kisabuni na kumjibu swaiba wangu usijali bro huyo ni mwanamke na between us k**a haiwezi kuvunja urafiki wetu.
Nilivyo achana na rafiki yangu huyo nikampigia simu mpenzi wangu huyo na kumwuliza kama kweli kanisaliti na nilitaka yeye ndo anithibitishie hilo.Mpenzi alikataa katakata basi ikabidi nimpotezee tu maana aliniongopea.
Miezi sita tukawa hatuna mawasiliano lakini tarehe mmoja January 2012 mida ya mkesha namba mpya ilinipigia.Nikaipoke na aliye nipigia alikua si mwingine bali ni yule mpenzi wangu.Akanisalimu na kunitakia heri ya mwaka mpya huku akiniomba turudiane tena na kukiri ni kweli alimpa mzigo mchizi wangu. Mi nilimwambia niliisha kusamehe mda mrefu hivyo asijali.Na kuhusu kua wapenzi tena haiwezekani labda abaki kua rafiki tu.Binti alikubali tukawa tunawasiliana Mara kwa Mara.
Mwaka huo wa 2012 nika maliza advance na kurudi mtaani nikisubiri matokeo.Kipindi chote hicho nikawa na onana na huyu Dada na kubadilishana mawazo mawili matatu.Kadri tulivyokua tunawasiliana tukajikuta tumerudi tena kwenye mahusiano.
Mwaka huo huo results zilitoka nikawa nimefaulu hivyo nikaapply university moja na kupata.Nikamuaga mpenzi wangu huyo na kumueleza avumilie miaka mitatu so mingi na akakubali.
Nilivyo kua chuo nikagundua mpenzi wangu huyo anatabia ya ulevi hivyo nikamkanya na kumwambia aache kabisa tabia huyo na akakubali.Na nilikua napata habari zake kwamba hajatulia nikawa namusa aachane na mambo ya kihuni afocus kwenye kujenga maisha cuz ye ni mama na baadae tutakuja kuishi pamoja hivyo haitopendeza nije ni muoe afu mtaa mzima ujisifie umemfunua sketi.Akaniambia ameenielewa na ana ahidi kujirekebisha.
2015 nikamaliza masomo yangu na kurudi mtaani na kuaanza kujishughulisha na ujasiliamali.Nikamweleza mwenzangu avumilie japo mwaka mmoja nijijenge kimaisha then inshaallah tutaishi pamoja na Mimi ntakua responsible katika kumtunza mwanae kama baba wa kambo .
Kinacho nitatiza sasa baada ya kujijenga na mambo yangu yameanza kuninyookea huyu binti kabadilika amekua anakibri na hataki kuelekezeka pale anapo kosea.Ananidharau na kuniona pimbi tu.Hata mawasiliano yamepungua na kila nikimtafuta hewani Mara nyingi huniambia yuko bize kidogo atanitafuta lakini unakuta ndo imetoka.
Mara kadhaa nimekua natamani nimpotezee tu lakini kila nikifikiria mda nilio upoteza nahisi itanigharimu mda mwingi kuanzisha mahusiano mengine.Ukizingatia mabinti wakuoa siku hakuna wengi wanatabia za hovyo hovyo.Na mimi nilisha mweleza binti huyu na nia ya kumuoa lakini toka niweleze hayo haonyeshi zile wife material characters. Anadai ananipenda lakini hajali,hanithamini hata nikijaribu kuzungumza nae she doesn't Care na hii inanivunja moyo sana.Nifanye nini hapa!?!? Ushauri wenu tafadhali.