Nifanye nini hapa?

Pole sana kak....ila kwa maono yangu huyo achana nae una moyo mzuri sana na kama hakukuelewa mpaka sasa....usiangaike nae accept tu yameisha na uendelee kujijenga mwenyewe mapenzi ndoa vipo tu.....omba mungu kila kitu kitakuja kwa wakati wake
Asante kwa ushauri mzuri.Mola akuzidishie.
 
Achana na huyo, mkuu utakuja juta bure. Sikh lazima umuoe huyo. Wanawake wapo wengi.
 
Mapenzi yanatakiwa yawe ya pande zote. Kuna jambo labda anakosa ujasiri wa kukuambia. Inawezekana alishampata mwanamme mwingine. Kwahyo, si ajabu anakufanyia visa ili wewe ndio umuache ili apunguze guilty consciousness. Au inawezekana ana tatizo tofauti kabisa ambalo anahisi ukilijua linaweza kuathiri mapenzi yenu and may be yuko scared kukupoteza hivyo anatafuta space ili alitatue kwanza. Jaribu kumface na kumuuliza nini kinachomsibu and then from there utapata majibu ya maswali yote magumu ili ufanye uamuzi sahihi.

Halafu mkuu nakukumbusha tu kuwa, kwa mtazamo wangu, katika mapenzi hakuna kitu muhimu kama kuheshimiana, kujaliana na kuthaminiana. Hivyo, vitu vitatu vikiwa havipo hata kama vingine vitakuwepo, basi mapenzi hayo yatakuwa ni maigizo tu na mwisho wake ni maumivu tu.

Wekeza muda wako kwenye kujijenga kimaisha lakini pia mkuu unaonekana ni muoga sana kuanza maisha upya bila huyo binti. Sikuambii ukimbilie kumuacha kabla ya kumpa nafasi (angalau ya mwisho) ya kumsikiliza, ila kama baada ya kusikia story yake utaona ni ujanjaujanja na usanii uleule wa siku za nyuma, usisite kuachana naye kwa amani. Usilazimishe penzi itakuja kukugharimu big time! Kila la kher mkuu na pole sana
 
Kwa mara ya kwanza leo ndio nimeona mwanaume akizingatia muda aliowekeza kwenye mahusiano. So dear ladies, let this go on record kwamba hata nyie huwa mnatupotezea muda.
 
Huu ndio upuuzi ambao nilisha sema siwezi ufanya aiseeee.....
Yaani unao ushahidi wa kuumizwa alafu unakuja kutuuliza nini ufanye..[emoji15]
Weulipaswa ufanye kitu, kisha ndipo uje hapa jamvini kutueleza nini kilicho jiri, kisha itafanya nini, na mwisho ikawaje.
Hii ingesaidia sana kukutuliza jakamoyo, na pengine wengine wangepata la kujifunza kupitia wewe, na hata ungeweza pata ushauri ulio sahihi.
Naona bado hajajua tofauti kati ya HUBA na MAHABA
 
Yaan wewe ni zaid ya pimbi, nitumie namba yake pm nam nikapone maana huyo ni kanyaga twende.
 

Wewe ndiyo mwenye tatizo... Ulitongozwa na huyu Binti ukaingia line.. Sasa mambo yako wazi siyo mke wa kuoa una shindwa utaanza je kutongoza maana Hujawahi kutongoza mwananake....
 
Unasema mabinti wa kuoa siku hizi hawapo kwa hiyo huyo ndo umemuona cream baada ya kusagulasagula? Mbona unawaonea hivyo mabinti yani hata hapo kijijini kwenu wote wana tabia mbaya kuliko huyo wa kwako?
 
Waswahili wanasema, "mapenzi ni kama kujaaamba, ukilazimisha sana utahaarisha!"
 
Yaani binti anakufanyia mizengwe yote hiyo hadi kutembea na rafiki yako halafu bado unakuja hapa kulalamika kama mtoto wa kike.Hivi kwanini mnatuaibisha wanaume marijali jamani?Bastar...d.
 
Yaani binti anakufanyia mizengwe yote hiyo hadi kutembea na rafiki yako halafu bado unakuja hapa kulalamika kama mtoto wa kike.Hivi kwanini mnatuaibisha wanaume marijali jamani?Bastar...d.
I understand your disappointment spot,lakini hukua na ulazima wa kunitusi....if you could wall a mile in my shoes you'd be crazy too.I came here kutokana na watu wengi humu be it males ama females ni watu wazima na wengine perhaps wanapitia mapito kama yangu au wamewahi pitia,so through experience yao Ninaweza jifunza kitu toka kwao kabla ya kufikia maamuzi yeyote.When a brother slip and fall don't vituperate him rather help him to his feet na umshauri njia ipi yaweza mfaa kama akipita.Insults like yours crushes a broken heart.
 
Unasema mabinti wa kuoa siku hizi hawapo kwa hiyo huyo ndo umemuona cream baada ya kusagulasagula? Mbona unawaonea hivyo mabinti yani hata hapo kijijini kwenu wote wana tabia mbaya kuliko huyo wa kwako?
Don't get me wrong hapo...yawezekana nimetumia kauli isiyo ya kistaarabu kwa dada zetu labda kutokana na mazingira.Kwa ninapo tokea wengi ni matatizo,katika kila akina dada 10 unakuta watatu wametulia.so mazingira nitokayo yame influence kauli yangu.Niwie radhi kwa hilo.
 
Unasema mabinti wa kuoa siku hizi hawapo kwa hiyo huyo ndo umemuona cream baada ya kusagulasagula? Mbona unawaonea hivyo mabinti yani hata hapo kijijini kwenu wote wana tabia mbaya kuliko huyo wa kwako?
Huyu sijui wa wapi aisee
 
Acha ufala, piga chini! Hujamuoa anakuzingua ukimuoa atakuua kwa pressure,
Kuna watoto wakali wako desperate kuolewa, vuta subira utampata wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…