Nifanye nini ili aniamini

marrykate

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2012
Posts
733
Reaction score
443
nilifahamiana na huyu kaka miaka kumi na mbili iliyopita, alisha propose mara tatu na zote sikukubali,na pia nimemfanyia vituko vingi sana ili akae mbali na mimi, miezi kama mitatu imepita siku moja nikanza kumuwaza in a positive way,nikakumbuka mazuri yake na kutamani niwe nae, uwezi amini the same day nawaza akanipigia simu nikaongea nae vizuri kwa utulivu mwingi, hakuamini kama ni mimi na usiku wa siku hiyo akanipigia tena na kupropose kwa mara ya nne, nilimkubalia, tupo kwenye mahusiano sasa hivi yamekolea balaaaa, ila mwenzangu ana wasi wasi mwingi kwamba naweza kumwaga muda wowote, na anataka anijaze mimba kabla sijabadili mawazo,sipo tayari kubeba mimba kabla ya ndoa

nifanye nini ili aniamini nampenda kwa dhati na sipo tayari kumpoteza. ili asubiri tufunge ndoa kwanza ndo nipate ujauzito
 
unaogopa mimba kuliko zinaa siyo? Ukimwi mmeshapima? Ingia kwenye ndoa naye aanze kukulipizia.... Chezeya sisi vidume?
khaaaaa! Yaani kumbe mnajijuaga kuwa mnatulipizia! Lol!
 
Kubali mimba! Kwanini hauko tayari kubeba mimba?
 
Unaogopa mimba kuliko zinaa siyo? Ukimwi mmeshapima? Ingia kwenye ndoa naye aanze kukulipizia.... Chezeya sisi vidume?

Asprin kama mwanaume atakuja kumtenda kwa nia ya kulipiza basi huyo ni shetani, ningependa kumwambia marykate aende akasome thread ya Mbu .....umethubutu asome post hiyo vizuri sana ataona what it takes to start maisha ya ndoa.

ila asijali wala msimuonyeshe upande mbaya wa maisha.
 
Last edited by a moderator:
Hua nasikia mwanaume ukimsumbua kwa mda mrefu sana akikupata lazima akukomeshe! Sijui kama ni kweli au lah!
 
marry kwanza hongera kwa kumpata mchumba. pia huyu nakuhakikishia ndiye mumeo wa kweli from god. HILI lina mfano wa dhahiri kabisa na kama unataka ushuhuda ni pm.

ila aausibebe mimba ma dear wala usizini jaribu kweli kucontai hisia za mapenzi kwanza ili mfunge kwanza ndoa. kumbuka marry tunategemea wachumba waoane wakiwa wote mabikira so hata kama huna usiiachie tena manake aweza kuipata pasi kutarajia ukajajuta na ukakuta umevunja mwiko wako. kwangu mimi naamin waweza kujitunza msifanye hadi siku ya honey moon na tena siku hiyo ukajikuta huwez ku do manake kidanguro cha weza kukuumbua. hebu tulia ma dearest

usipende kukaa naye sehem za faragha ama kumtembelea home kwake utajikuta umezini tu onana naye mahali pa wazi kisha kila mtu achukue time
 
nashangaa kwa nini wanawake wanaogopa sana mimba kabla ya ndoa, mbona sielewi? Why?

Yaani yuko radhi azichomoe hadi aolewe au asubiri hata afikishe miaka 40 hazai wakati anapenda watoto.

Ndoa si suluhisho, ni bora kuwa kwenye mahusiano yenye afya hata kama si ndoa kuliko kukalia kuti kavu ndoani.
 
Kama mshkaji anaharaka sana si mfunge ndoa tu hata kesho au wewe unamuwekea pingamizi akitaka kukuoa fasta fasta?
 
Rutta,what if Marry is your very own daughter,utamshauri hivi?

hawezi kuomba ushauri huu kwa baba yake!
Kama hana sababu yakuto beba mimba kwa nini asibebe!
 
Kila jambo na wakati wake ndoa huleta watoto, kipi kianze any of the two kwa dunia ya sasa cyo ishu ila kwa heshima ndoa ianze.
 
nilifahamiana na huyu kaka miaka kumi na mbili iliyopita,
duh miaka kumi na mbil iliyopita nilikuwa form 1 kudadek jamaa bnamoyo kweli mi mwanamke miez 3 tu inatosha kukuvutia punzi else natupa kule then kipind chote icho lazma ntapunguza kujiamin ata kama nitakuwa nawewe .jichek jamaa anawez kukupa kibut cha aja umlele mtoto peke yako .ogopa mbwa koko akipata upenyo ata ikibidi kung'ata atang'ata ili aponye nafsi yake
 
vibinti vinaogopa mimba kuliko dhambi na ukimwi lol

mimba phobia

yaani mwanamme nikimtamani tamani tu, nambebea mimba lol

mayai yenyewe mnayabania wakati hata kwenye chips hayauziki.

Nimebakiza kupata mimba ya Bishanga tu
 
Last edited by a moderator:
vibinti vinaogopa mimba kuliko dhambi na ukimwi lol

mimba phobia

yaani mwanamme nikimtamani tamani tu, nambebea mimba lol

mayai yenyewe mnayabania wakati hata kwenye chips hayauziki.

Nimebakiza kupata mimba ya Bishanga tu

shemejiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Last edited by a moderator:
kubeba mimba sio kumwaminisha, mpe muda, mfanye ajisikie kweli umezama....... Na mwambie akuamini....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…