Unatakiwa kuandika barua(notice) ya siku 30 kwa mwajii wako kumjulisha kuwa asitishe kukukata michango ya trade unioni kuanzia tarehe fulani ambayo utaitaja, nakala ta barua hiyo utaipeleka kwa cwt, hapo itakuwa ndy mwisho wa kukatwa
Usimdanganye, yeye lazima awe member wa chama cha wafanyakazi kinachofanana na taaluma yake.
Na atakapojitoa aainishe chama anakojiunga kwa kuwa TUCTA hukata asilimia 1 ya makato hayo ya vyama vyote na hilo ni takwa la kisheria duniani chini ya ILO.
Kuna mambo watu wanakesha kuhangaika nayo hadi wanaacha miradi yao inadorora kisa vyama vya wafanyakazi.
Nilichogundua wapinzani wakuu wa cwt wengi waligombea vyeo wakashindwa.
Wewe una miradi yako,una mshahara wako haufyekwi wote ukae unapoteza muda kwa 2%.
Pia watu tumieni akili.Hivi toka mtu umeajiriwa ukaambiwa mshahara wako bado kuna nyongeza na marupurupu yameendelea kuongezeka kila mwaka bila ya wewe unadhani anayesimamia yote hayo ni nani?.
Kuna chama cha waajiri Tanzania hata duniani pia wao hujadili namna ya kumkandamiza mwajiriwa sasa leo watu mnapanga namna ya kuua vyama vyenu.
Huenda kweli cwt ina mapungufu lakini pia cwt ni nzuri kuliko vyama vingi vya wafanyakazi shida ni uwingi wa member wake maana mnapata tshirt bure idara nyingine ni kununua,mnapata return ya pesa yenu kila mwezi mahali pa kazi wakati idara nyingine hicho kitu hakuna,mmewekeza majengo ambayo kama mtapata uwekezaji mzuri mbeleni ni balaa wakati vyama vingine wanakusanya pesa hata ofisi makao makuu ni shida achilia mbali mikoani na wilayani,mmeajiri watendaji kila wilaya ,mkoa hadi taifa na wana walinzi,magari,stationery, wahasibu,makarani,usafi na wanalipwa mshahara ambao ni sehemu ya makato ya pesa yenu bado hamuoni.
Walimu mna ujinga mkubwa wa kutoelewa.Kama hamjui kwa sasa idara zote Tanzania tunafaidi matunda ya benki yenu kwa sababu kuu zifuatazo.
1.Walimu mnazifaidisha benki zote kwa 65% kwa kuwa ndiyo wakopaji wakuu.Bila walimu nmb ingekufa kabisaa.Mlipopata benki yenu mkashusha riba hadi 17 benki zote tz zimelazimika kushusha riba hadi 17 toka 26 huko na tusio walimu nasi tumefaidika kupitia ninyi.
Kwa kushusha riba tu kwa mkopo uleule nimeenda kuurenew nimepata ongezeko la milioni 7 bila kubadili makato Mungu akupe nini ila,najua bila benki ya cwt isingetokea hii.
2.adui wa mwalimu ni mwalimu mwenyewe, wengi wenu walimu hamjui dhamira ya chama hivyo hakuna mnachoweza kupongeza kila kitu mtakiponda tu hata kiwe chema.Viongozi wenu wengine wamefukuzwa kazi wakiwatetea ninyi lakini nyie mpo mtaani kuwaponda.Mfano halisi yule msabato mwl . OLOUCH hayupo kazini lakini bila yeye walimu wakuu wasingepata posho ya madaraka laki 250000/= kila mwezi leo hamkitaki chama chenu eti muondolewe makato.
Jifunzeni kubadilika siyo kila unachokifanya utafaidika nacho 100asilimia.Itunzeni cwt ina malengo ambayo yametusaidia watumishi wengi hata tusio cwt.Hiyo benki ikiwa imara itakomesha benki nyingi nchini kama ilivyo sasa.