Nifanye nini ili niache umbea

Nifanye nini ili niache umbea

Ninapenda sana kujua habari za watu, kuanzia macelebrity mpaka majirani zangu. Ninapenda kusoma habari hizo mitandaoni mpaka kwenye magazeti. Ninaweza kununua gazeti sh10,000 mradi tu nijue Oprah amefanya nini wiki hii. Ninataka niachane na ki tabia hiki.
Hilo ni Pepo. Ni sawa Na kukaa barazani pa wenye mizaha. Biblia imetukaza.
Soma Zaburi Mlango 1

1 Heri mtu yule asiyekwendaKatika shauri la wasio haki;Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
 
Mm sioni kama kuna shida saana hapo karibu kila mwanadamu ana tabia kama yako ila kwa kiwango tofauti , kwa ku proove hilo ndio maana Tasnia ya habari ndio chanzo kikubwa cha utajiri , matajiri wengi wa dunia yetu wanamiliki vyombo vya habari,kupenda kujua nn kinatokea duniani inaonyesha jinsi gani ulivyo up to date, tatizo linakuja pale unapoitumia hiyo habari kwa makusudio tofauti. kupenda kujua yanayotokea kwa majirani pia sio mbaya ubaya ni pale unaposambaza yale uliyoyajua kwa mtazamo HASI.
Nikikuangalia kwa jicho la jingine wewe ni mwanahabari by nature ila hujakitambua kipaji chako!usikwazike na maneno ya watu wote tuliomo humu JF tuna tabia zinazokaribiana na zako tunapenda kujua nini kinatokea duniani mpk kwa jirani zetu vinginevyo hii forum isinge exist.
 
Ninapenda sana kujua habari za watu, kuanzia macelebrity mpaka majirani zangu. Ninapenda kusoma habari hizo mitandaoni mpaka kwenye magazeti. Ninaweza kununua gazeti sh10,000 mradi tu nijue Oprah amefanya nini wiki hii. Ninataka niachane na ki tabia hiki.
[emoji23]
 
Aisee pole na hongera kwa kujua udhaifu wako maana ni wanawake wachache tunaokubaligi madhaifu yetu

Sasa basi jitahidi kupunguza kufatilia mambo hayo ya watu hasa majirani yaani jifunzw kupuuzia natamani nikupe tabia hii ya kupuuza

Pole madame no one is perfect mi nakukubaligi na hii imefanya nikukubali zaidi
 
Kuwa busy na shughuli zako mchana kutwa,ikifika usiku utalala fofofo kwa uchovu. Kukicha tena busy.......utajikuta huna muda na umbea.
 
Mm sioni kama kuna shida saana hapo karibu kila mwanadamu ana tabia kama yako ila kwa kiwango tofauti , kwa ku proove hilo ndio maana Tasnia ya habari ndio chanzo kikubwa cha utajiri , matajiri wengi wa dunia yetu wanamiliki vyombo vya habari,kupenda kujua nn kinatokea duniani inaonyesha jinsi gani ulivyo up to date, tatizo linakuja pale unapoitumia hiyo habari kwa makusudio tofauti. kupenda kujua yanayotokea kwa majirani pia sio mbaya ubaya ni pale unaposambaza yale uliyoyajua kwa mtazamo HASI.
Nikikuangalia kwa jicho la jingine wewe ni mwanahabari by nature ila hujakitambua kipaji chako!usikwazike na maneno ya watu wote tuliomo humu JF tuna tabia zinazokaribiana na zako tunapenda kujua nini kinatokea duniani mpk kwa jirani zetu vinginevyo hii forum isinge exist.
Asante sana, ni muhimu kufahamu yanayoendelea katika jamii. Wengi wameona maambukizi ya UKIMWI baada ya kusikia tetesi kuwa Fulani ni muathirika na kukaa nae mbali.

Jinsi unzvyoitumia information ndiyo what matters. Shukran mkuu.
 
Back
Top Bottom