Nifanye nini ili niweze kuingiza laki mbili kwa wiki nje ya mshahara?

Hahahahaha ukiskia watu wanapiga hela bisharani usidhanie kipompi pompi!
 
Hii naweza sema nakubaliana na wewe maana biashara zinazoonekana za kudhalilisha utu ndio huwa na faida maradufu.
Ndio biashara pekee ambazo zinatumia mitaji midogo ila zina faida kubwa kwa haraka sana maana gharama za kuuzia zipo chini.
Ila kibongo bongo kila mtu anataka amiliki duka la nguo ndio ajihisi ana biashara. Mtu akibutua tu Million zake kadhaa zote anatia kwenye duka la nguo ambako turnover ni ndogo sana.

Laiti watu wangejua vitu vya 500-1000 vinaweza kuuzika kwa wingi na urahisi kuliko vitu vya 20,000-100,000 kwa siku basi wengi tungekuwa mbali sana. Sema ndio hivyo vitu vya jero mpaka buku ndio tunaona biashara za kudhalilisha utu.

Bhakresa sio chizi kuuza juice, maji na soda za 600-1000. Angeweza hata kufungua woolworth yake bongo hapa ila kwa kufuata kwake kanuni za biashara tutaendelea kumpigia makofi kila siku.
 
Amesahau kuwa hio ilikuwa awamu ya mkwere!
 
Kaba
 
Hv hawa wachina wanaonunua mabondo wanapatikana wapi???

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Endapo mtu anataka kuwekeza pesa zake kwako. Unatoa riba asilimia ngapi?

Mfano, mtu akikupa 3M, utampa kiasi gani kwa mwezi? Kumbuka wewe ndio unaefanya hiyo kazi ya kuzalisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…