Nifanye nini kukomboa chombo changu cha moto?

Nifanye nini kukomboa chombo changu cha moto?

Novida

Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
40
Reaction score
13
Habari wana jukwaa,

Nina pikipiki ya kutembelea ambayo nilikua namiliki kabla ya kumachia rafikiyangu anihifadhie kwa kipindi ambacho nilisafiri. Naye akampitia mtu asiyekua na lesen ili aendeshe. Kwa bahati mbaya mtu aliye pewa pikipiki alisababisha ajali ambapo alimgonga mtu na kumtengua mguu ingawa mwenyewe alisema mguu umevunjika. Pikipiki ilikamatwa na kupelekwa kituoni.

Nilipo ifuatilia nikatakiwa nimpeleke mtu niliye mkabidhi, ndipo akawekwa chini ya ulinzi na kukamatwa kwa kumkabidhi chombo cha moto mtu asiye na lesen. hadi sasa watuhumiwa (aliye sababisha ajali na aliemkabidhi pikipiki) wapo nje kwa dhamana. Nilipo endelea kufuatilia pikipiki yangu, Nilieleza ukweli wa makosa ya pikipiki yangu kwa mkuu wa kituo, akaniambia nisubiri niandikiwe makosa nilipe faini kitu ambacho nilikua tayali kukitekeleza.

Nikamfuata askari alie kua anahusika kuandika makosa, akaniambia niende kwa askari aliye ikamata pikipiki yangu kwani ndiye anaye tambua makosa yangu. Nilipo mfuata yule alie ikamata akakataa. nikamueleza kua makosa yote mkuu anayajua na amsema niandikiwe makosa yangu ili nilipe fain. Afande huyo alinituma nikamuulize mkuu kwamba waniandikie makosa gani? Swali ambalo lili mkera mkuu na kumuita afande yule.

Afande alipo ulizwa kwann hataki kunipatia pikipiki yangu ilihali nipo tayari kulipia faini? akaseama pikipiki haitoki hadi kesi itakapo fika mahakamani. Mkuu aliuliza iwapo kesi imesha funguliwa Askari yule alisema kesi imesha funguliwa ilihali kesi haijafunguliwa mahakamani hata mlalamikaji (aliye gongwa) hana mpango wa kufungua kesi isipokua anaombatu apone salama na hana tatizo na mtu.

Mkuu alipo ambiwa kesi imesha funguliwa akaniambia nusubiri kesi ingawa mimi sihusiki na kesi ile Samahani sana wana jukwaa kwa maelezo marefu. Naomba kwa anae elewa sheria au utaratibu nifanye nini ili nipate pikipiki yangu maana imemaliza mwezi nina subiri kesi ikiwa mlalamikaji hayupo teyari kufungua kesi?
 
vyombo vya moto ni shida hasa hizi pikipiki.yalishanikuta kama hayo nikaamua kuziuza zote
 
Kwanza pole kwa mkasa huo; pili fanya moja kati ya haya;
1: Penye kadhia penyeza rupia; afande anatengeneza mazingira ya kukutoa mpunga! ongea nae kwa uwazi; mkatie kitu kidogo atakupa tukutuku yako; au
2. Samehe 7x770! inauma na ni ngumu sana lakini Mungu aliyekupa mwanzo atakupa faraja utapata maradufu; mchuma hivi, kigari!
 
Huyo afande ananjaa na wewe umeshindwa kumuingia..
In short huyo anataka fungu ..so cha kukushauri chukua namba yake then mkutane kivulini bar acha kujifanya mbahili huku ukiendelea kukompliketi mambo!
 
Kwanza pole kwa mkasa huo; pili fanya moja kati ya haya;
1: Penye kadhia penyeza rupia; afande anatengeneza mazingira ya kukutoa mpunga! ongea nae kwa uwazi; mkatie kitu kidogo atakupa tukutuku yako; au
2. Samehe 7x770! inauma na ni ngumu sana lakini Mungu aliyekupa mwanzo atakupa faraja utapata maradufu; mchuma hivi, kigari!

Ilifikia hatua ya kudai pesa alikua tayari kuitoa lakini kwakua alisha vuruga kwa mkuu, siku alipo omba funguo ili anipatie pikipiki mkuu akamwambia "Si ulisema hadi mfikishane mahakamani" ndio ikawa ugumu tena.
 
Hapa kuna mawili kaka.

1. Unaweza ukatoa "kibubu" kwa maafande wote hao wawili, yakaisha, au

2. Andika barua kwa Mkuu wa Trafiki wa Kituo Husika, kisha weka nakala kwa watu hawa wafuatao:

a) Kama uko Dar es Salaam, nakala 1 weka kwa Mkuu wa Trafiki wa Wilaya na nakala ya 2 iweke kwa Mkuu wa Trafiki wa Mkoa

b) Weka nakala 1 kwa IGP na nakala nyingine 1 weka kwa Ofisi ya Mkoa/Wilaya ya PCCB.

Kisha kaa usubiri na kusikilizia moto wake.

Hawa jamaa huwa wanajifanya wajanja, haswa katika ngazi za chini. Wanatugeuza sisi raia kuwa mradi wao. Lakini ukiandika barua kulalamika ngazi za juu, utaona jinsi watakavyoogopa. Hawapendi kabisa mambo yafike huko juu, kwani wanakuwa wanawaumbua na kuwaaibisha viongozi wao wa juu.

Kwa mujibu wa "kanuni zisizo rasmi" ndani ya Jeshi la Polisi, ni "kosa la jinai" au "utovu wa nidhamu" kwa askari wa ngazi ya chini "kushindwa kumalizana" na "mteja wake" (wewe hapo) na kusababisha mambo yaende ngazi za juu.

Niliwahi kuandika barua iliyomfukuzisha kazi askari mmoja wa cheo cha Inspekta. Kwa hiyo tumia kalamu yako. Kama huwezi kuandika vizuri, tafuta mtu akusaidie kurekebisha vizuri lugha, ieleweke kwa wepesi na ufasaha.

Kila la heri.
 
Back
Top Bottom