Njuka II
JF-Expert Member
- Feb 25, 2019
- 414
- 733
Kawaida maji huwa tunayacontrol kwa kutumia slope (muinuko). Sasa huko juu ili maji yasikae kwenye kuta ambayo yanafanya yafyozwe na tofali zinazofata wakati mvua inanyesha, tengeneza slope ndogo kwenye copping inayozunguka nyumba na sio lazima iwe ni slope ya kuonekana kwa macho, hata kukiwa na utofauti wa milimita 2 tu itatosha kuyaelekeza maji yaende mahali unapotaka yaende...kama ulishawahi kuona nyumba za contemporary utaona kule juu kuna kozi moja ya tofali huwa inalazwa mara nyingi huwa zinatumika tofali za nchi 4 japo wengine hupendelea kutumia zege mana zege haifyonzi maji mengi kama ilivyo kwa tofali (hii ndio tunaita copping wall). Wakati unaweka hiyo slope yako usisahau kuweka water proof kwenye udongo wako (wengine huwa wanapaka nilu kabisa).Vp nkibandika kigae mkuu au puty?
Vipi kuhusu maji kuingia dirishani? Ukijenga contemporary ni vizuri ukaweka window cap (hii huwa tunaioteshea kwenye mkanda) ili kuzuia maji yanayotembea kwenye ukuta kuingia dirishani vinginevyo itakulazimu utoboe vitundu vidogo kwa nje kwenye alumunium case ili maji yasijae kwenye hako kamfereji ambapo vioo vinapita na kuingia ndani ambapo inaharibu muonekano ya dirisha