Nifanye nini niache kukataliwa, nianze kupewa nafasi kazini au kwenye fursa mbalimbali?

Nifanye nini niache kukataliwa, nianze kupewa nafasi kazini au kwenye fursa mbalimbali?

Kibenje KK

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2016
Posts
270
Reaction score
391
Kama una tatizo katika mwili wako na inahitajika ufanyiwe upasuaji (operation/surgery).

Na wakawepo watu wawili, mmoja ni rafiki yako wa karibu unayempenda lakini hana utaalamu wowote juu ya upasuaji na mwili wa binadamu lakini wa pili ni mtaalamu na ana uwezo mkubwa wa upasuaji kutokana na operesheni nyingi alizofanya zikafanikiwa.

Je, utamchagua nani kati yao akufanyie upasuaji?

Ni lazima utachagua mwenye uwezo mzuri na utaalamu wa upasuaji.

Imetokea umeanzisha Kampuni. Ndugu/Rafiki yako akaja anahitaji kazi, akaja mwingine hujui lakini ana uzoefu na teknolojia, ana ujuzi wa masoko na ushawishi kwenye biashara, ana uelewa juu ya sheria za biashara. Utachukua nani kwenye wawili hawa?

Hivyo hivyo kwenye fursa mbalimbali zinazotokea.

Hakuna mtu anayeweza kukupa fursa inayozidi uwezo wako kisa tu anakujua.

Yaani unapata fursa kulingana na uwezo wako. Ukiwa na uwezo wa kufundisha Shule ya msingi hakuna atakayekupa nafasi ya kufundisha chuo kikuu.

Ukiwa na uwezo wa kuchezea timu ya Mtaani huwezi kuchezea ligi kuu Uingereza.

Unapata nafasi kulingana na uwezo wako. Ukitaka nafasi za juu na fursa kubwa kubwa ni muhimu kuongeza uwezo wako pia kuwa mkubwa.

Hakuna mtu atakudharau kama una uwezo mkubwa wa kufanya jambo kwa ufanisi.

Watu wengi tunagusagusa vitu tu. Hatuna muda wa Kujenga uwezo na kuwa experts, tunakaa kulilia na kulaumu connections.

Ukiongeza uwezo no one can ignore you.

ONGEZA UWEZO

Watu wakujue na wakugombanie sababu uko vizuri katika eneo fulani.

#begood #kelvinkibenje
 
Back
Top Bottom