Binafsi nilishawahi Kuwa na wazo Kama lako wakati nikiwa chuo Kikuu..
Nilipokuwa first year nilipanga pindi nimalizapo chuo nifungue company yangu binafsi au organization..
Lakini ktk mwaka huo huo first year nilibahatika kufanya field ktk organization flani, nilikuwa inspired jinsi wanavyofanya kaz maana ilikuwa target yng baada tu ya kumaliza masomo nifanye Kaz kwny company/organization yangu...
Lakini nilifikiria nikaona ili company / organization yangu ikue itanihitaji alteast 2years to 3years... Nikaona hiyo miaka miwili au mitatu nitakua nafanya nini baada ya kumaliza chuo wakati nikisubiri ku raise profile ya organization/company.
Nilipofika mwaka wa pili nikaamua rasmi kuanzisha na kusajili taasisi yangu ili iweze ku-compensate miaka 2 ijayo ili kukuwa na kufahamika... Niliomba baadhi ya classmates wangu kuungana nami lakini wote hawakuwa tayari maana waliona hakuna manufaa yoyote wangeyapata kwa kipindi hicho...
Kwasababu ilikuwa comfort zone yangu nikaamua kutumia Pesa yangu ya matumizi kutengeneza katiba + kusajili + kudesign website...
Baada ya hapo nilikuwa natumia muda mwingi kuipromote na kupost kwenye website makala zangu (zilikuwa inahusu changamoto zinazokabili jamii yangu)
Nikiwa mwaka wa 3 nilipata fursa ya kufanya kazi kupitia organization yangu in partnership na organization nyingine kubwa...
Nilianza ku-earn japokuwa kidogo sana hasa katika seasonal projects, kupitia hizo project nilipata kiasi Fulani cha Pesa nikaamua kununua piki piki 2, 1 kwa ajili ya matumizi yangu, nyingine nikamkabidhi mtu kwa ajili ya kuifanyia biashara...
Lakini baada ya miezi kadhaa niliuza piki piki kulingana na usumbufu niliokuwa na upata kutoka kwa mtu niliyempa kufanya biashara (in short hakuwa mwaminifu na hakuwa makini )
Nilipokuwa mwaka wa mwa mwisho chuo (fourth year, nimesoma Engineering) nilianza kupata wasiwasi juu hatima ya maisha yangu baada ya kumaliza chuo maana sikuwa na stable financial katika taasisi yangu, nikiwa nimebakiza mwezi mmoja kumaliza chuo niliapply kazi sehemu fulani nikaitwa interview.. Katika interview Mimi ndio nilikuwa mdogo kuliko wote na alikuwa anatakiwa mtu mmoja.
Kwa bahati nzuri nipata ile nafasi na nikafanya kazi kama miezi 3 nikaacha maana haikuwa comfort zone yangu na nikaona taasisi yangu inakufa kulingana kuwa busy na kazi kuliko kuendeleza taasisi.
Kuanzia hapo sijawahi kuomba kazi sehemu yoyote lakini ninaishi kupitia kufanya kazi kwenye taasisi yangu japokuwa bado ndogo inaendelea kukuwa.
Negative Impacts nilizokumbana nazo kulingana na maamuzi yangu:-
1. Attendance yangu darasani ilipungua hivyo performance yangu ilishuka japokuwa sikuwahi kupata surp hata 1
2. GPA yangu haikuwa nzuri sana, ilikuwa moderate, nilikuwa na 2nd class.
3. Idadi ya marafiki ilipungua sana maana muda mwingi nilikuwa busy na mambo yangu
4. Nilikuwa naongoza kwa kuzima moto darasani maana muda mwingi nilikuwa busy..
Nimeshare experience yangu kidogo ila sikushauri ufate kama Mimi nilivyofanya lakini jambo la msingi angalia Comfort zone yako ni ipi na sio copying & paste
Sent using
Jamii Forums mobile app